Rais Yoweri Museveni amewaonya wananchi wa Uganda dhidi ya vitendo vya kutumia mdomo katika kufanya mapenzi, akisema "mdomo uliumbwa kwa ajili ya kula na si mapenzi".
Rais huyo wa muda mrefu nchini Uganda amesema utamaduni huo wa kutumia mdomo katika mapenzi uliletwa na wageni.
“Nichukue nafasi hii kuonya watu wetu hadharani dhidi ya vitendo visivyo sahihi vilivyoletwa na vinavyoendelezwa na wageni. Mojawapo ni mapenzi ya kutumia mdomo. Mdomo ni kwa ajili ya kula si mapenzi.” Museveni alisema hayo wiki iliyopita wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni.
Vyombo vya habari vya Uganda vimeripoti onyo hilo na kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii, ambako baadhi ya watu wanapingana naye na wengine kumpongeza.
Kauli yake ilitoka siku chache baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonyesha ofisa mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Makerere akimnyonya sehemu za siri mwanafunzi wake ofisini kwake.
Ofisa huyo, anayehusika na utawala, ameshasimamishwa kazi na analipwa nusu mshahara, wakati tukio hilo likichunguzwa.
Tukio hilo lilijulikana baada ya mwanafunzi huyo kusambaza picha alizojipiga wakati ofisa huyo akimfanyia kitendo hicho.
Mwanafunzi huyo alisema ofisa huyo wa Makerere alimbusu sehemu zake za siri kwa nguvu na alipiga picha hizo ili apate ushahidi kwa kuwa ofisi hiyo haikuwa na kamera za usalama.
0 comments:
Post a Comment