Mwanadada Monalisa ambae ni msanii mkongwe sana katika tasnia ya filamu amekabidhiwa bendera ya taifa pamoja na ticket ya ndege na Mh waziri wa michezo Harrison Mwakyembe kwa ajili ya safari yake ya kwenda Ghana ambapo ataenda kuepeperusha bendera ya Taifa katika maswala ya tasnia ya filamu kutokana na kuchaguliwa kwake katika kuwania tuzo za African Prestigious Award nchini humo zitakazofanyika April 14,2018 .
Monalisa ambae alisindikizwa na mama yake katika makabidhiano hayo katika ofisi za Baraza walihudhuria pia watu mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Habari sanaa na Michezo Mh .Juliana Shonza pamoja na katibu mtendaji wa baraza la sanaa tanzania.
Monalisa anakwenda kuiwakilisha Tanzania baada ya kuchaguliwa katika kategoria hiyo na kuomba watanzania na afrika kwa ujumla kumpiagia kura kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja sasa.Kila la kheri kwake.
0 comments:
Post a Comment