Msanii wa nyimbo za injili nchini , Madam Florah ambae hapo awali alikuwa akijulikanakana Florah Mbasha ameamua kumjibu mzazi mwenzie , ambae pia alikuwa mume wake wa ndoa Emmnanuel Mbasha kuhusu lawama zake alizokuwa amemtupia katika mtandao wa instagram siku ya wanawake duniani kuhusu kumnyima kumuona mtoto.
Madam Florah ameieleza Global Publisher kuwa hawezi kuzungumzia maswala nyeti kama hayo katika mitandao ya kijamii, wala katika vyombo vya habari juu ya swala hilo kwa sababu hata kama Emmanuel aliruhusiwa kumuona mtoto na mahakama lakini hakuruhusiwa na mahakama hiyo kuandika instagram,kwaio hawezi kuyasema hayo huko.
"Siwezi kuzungumzia hilo swala katika vyombo vya habari hata siku moja,hilo swala ameliongelea instagram na mimi ningelitolea instagram, na ukweli hamuujui ila sisi ndio tunaujua ukweli.na kama mahakama iliamua hivyo na yeye kaamua kuandika instagram basi sawa acha aandike ila siwezi kuliweka wazi.
Emmanuel Mbasha na Flora walibahatika kupta mtoto moja kipindi cha ndoa yao , lakini walipokuwa wanapeana talaka mahakama iliamuru mtoto akae na mama yake kutokana na umri wa mtoto na baada ya hapo Madam Florah aliamua kuolewa na mwanaume mwingine.
Hivi siku za karibuni emmanuel alifunguka katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa mama wa mtoto huyo amekuwa akikaidi agizo la mahakama la kumruhusu yeye kumuona mtoto na kusema kuwa hana njia nyingine yoyote ya kumtumia ujumbe Florah zaidi ya hiyo ya instagram.
0 comments:
Post a Comment