Home » » Dogo Janja afunguka sababu ya kupangiwa ratiba ya 'unyumba' na mkewe.

Dogo Janja afunguka sababu ya kupangiwa ratiba ya 'unyumba' na mkewe.

Unknown | Monday, March 12, 2018 | 0 comments
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja ambaye ni mume halali wa muigizaji wa filamu bongo Irene Pancras Uwoya, ameweka wazi sababu za kupangiwa ratiba na mke wake huyo, jambo ambalo lilizua kizaa zaa baada ya kuiweka kwenye mtandao.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo Janja amesema alishtuka baada ya kuona ratiba hiyo imebandikwa ukutani alipoamka, na kueleza sababu zake.

“Nilikuwa nimelala nimeamka nikakutana na ratiba kwenye ukuta, nikaangalia duh!! nikaipost insta. Unajua yule ni mshkaji wangu sana alikuwa ananitania, na yeye ndiye alianza kuipost, na kimvua hiki uniambie ratiba!!? Atadondoka mtu”, amesema Dogo Janja

Wawili hao walifunga ndoa ya kimya kimya jambo ambao wengi hawaamni mpaka leo kuwa ni wanandoa, na pia kutokana na tofauti ambazo wanaonekana wanazo za kiumri.

Advertisement
==
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG