Waandishi wa habari wa radio za Kijamii nchini Tanzania
wametakiwa kuzingatia maadili ya taaluma zao ili kuandika habari zenye weledi
katika kuzisaidia jamii zinazowazunguka.
Wito huo umetolewa leo mjini Dodoma na Mkufunzi
wa musuala ya habari kutoka shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na
utamaduni(UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu kwenye mafunzo ya siku nane
yanayoendelea kwenye ukumbi wa wakala wa
majengo (TBA).
Bi. Rose amesema ili jamii inufaike na uwepo wa radio
za Kijamii, waandishi wa habari wanatakiwa kuzingatia miiko na misingi
inayowaongoza katika Kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya umma na wao binafsi.
Kwa upande wao waandishi wa habari wa radio za
kijamii wamelishukuru shirika la UNESCO na kuongeza kuwa mafunzo hayo yatawasidia
katika kuboresha utendaji wao wa kazi katika vituo vyao.
Shirika la unesco linaeendelea kutoa mafunzo ya
uandishi wa habari kwa radio za kijamii nchini
ili kuwajengea uwezo wa kuandaa habari na vipindi vyenye ubora.
tazama picha za washiriki:-
tazama picha za washiriki:-
0 comments:
Post a Comment