Home » » RC Atumbua watumishi 44 kwa Kujihusisha na Siasa

RC Atumbua watumishi 44 kwa Kujihusisha na Siasa

Unknown | Tuesday, February 06, 2018 | 0 comments
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, ametengua nafasi za watumishi 44 wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu  baada ya kujiridhisha na tuhuma za kujihusisha na masuala ya siasa badala ya kutekeleza majukumu ya kiutumishi

Bw. Mnyeti ametengua nafasi hizo na kumkabidhi Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Arnold Msuya, orodha ya majina ya watumishi hao wakiwemo baadhi ya watendaji wa Vijiji na Kata, na kusema hatua ya watumishi hao kujihusisha na siasa imekwamisha shughuli za maendeleo.
Mkuu huyo wa Mkoa ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG