Serikali
imesema mradi wa uchimbaji mafuta katika Kisima kilichoanishwa
kuchimbwa kwenye eneo la kijiji cha Ipera Asilia, kwenye hifadhi tengefu
ya bonde la Kilombero, mkoani Morogoro, unatarajiwa kuanza rasmi mwezi
Septemba, 2018 ambapo kisima hicho kinakadiriwa kuwa na mafuta kuanzia
lita milioni 180 hadi 200.
Akizungumza
jana Februari 2, 2018 katika kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao
cha nne cha mkutano wa 10 wa Bunge mjini Dodoma, Waziri wa Nishati,
Dkt. Medard Kalemani amesema kinachosubiriwa ni kibali kutoka Baraza la
Mazingira nchini (NEMC) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania
(TAWA), ili uchimbaji huo uanze rasmi.
“Mkataba
ulishasainiwa tangu mwaka 2012 kilihobaki ni utekelezaji wa uchimbaji
na ugunduzi wa mafuta, mafuta yanayotarajiwa kuchimbwa kwenye eneo hilo
yanafikia milionii 180 hadi 200, mtaji ni mkubwa na utakua na manufaa
kwa wananchi wako na nchi kwa ujumla,” alisema na kuongeza.
“Kinachosubiriwa
ni kibali cha mazingira kutoka NEMC na mamlaka ya TAWA, mwezi Julai
mwaka huu tumehakikishiwa mkataba utapatikana na Septemba uchimbaji
utaanza rasmi.”
Serikali
kupitia shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) liliingia mkataba wa
utafiti na uchimbaji wa gesi na uvunaji mafuta na Kampuni ya Mafuta na
gesi ya Swala (Swala Oil), ambapo katika utekelezaji wa mkataba huo
iligundulika kuwepo kwa wingi mafuta ya petrol na gesi katika vijiji vya
Mtimbira.
0 comments:
Post a Comment