Waziri
wa katiba na sheria Profesa. Palamagamba Kabudi amesema Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ana mamlaka yote ya kutoa maagizo
kwa Mawaziri ambao wapo ndani ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri
Kabudi ametoa ufafanuzi huo leo (Jumanne) katika mkutano wa 10 kikao
cha sita cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu
swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge Juma kombo Hamadi alipotaka kufahamu
Rais Magufuli ana mamlaka gani kikatiba ya kutoa maagizo kwa Waziri
aliyepo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
"Rais
wa Muungano wa Tanzania anayo mamlaka ya mambo yote yanayohusu Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kama nchi huru", amesema Prof. Palamagamba.
Pamoja
na hayo, Prof. Palamagamba ameendelea kufafanua baadhi ya mambo kuwa
"katika masuala yote yanayohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkuu wa
nchi ni mmoja tu tena ambaye ni Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na yeye
peke yake ndio Amri Jeshi. Hakuna mtu mwingine yeyote wa kuyaamuru
majeshi ya Tanzania isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa sababu yeye ndio kiongozi mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania".
Kwa
upande mwingine, Prof. Palamagamba amesema Rais wa Zanzibar ni wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwenye heshima na hadhi ya urais kwa
mambo yote yasiyokuwa ya Muungano yanayohusu Zanzibar ambapo pia ni
Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
nafasi yake hiyo.
0 comments:
Post a Comment