Home » » Nassari afikishwa mahakamani Arumeru

Nassari afikishwa mahakamani Arumeru

Unknown | Tuesday, February 06, 2018 | 0 comments
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru akisubiri kusomewa shitaka linalomkabili.

Nasari amesema jana alikwenda Kituo cha Polisi Usa River kufuatilia silaha yake iliyochukuliwa na askari wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014.

Nassari amesema alipofika polisi alielezwa kuwa ana kesi ya kumshambulia mtendaji kosa analodaiwa kutenda mwaka 2014 .

Sheki Mfinanga ambaye ni wakili wa Nassari amesema hajui mteja wake anakabiliwa na shtaka gani.

"Jana walisema alishambulia lakini hatujui leo anashitakiwa kwa kosa gani ndiyo tunasubiri," amesema.

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG