Home » » Mlima Kilimanjaro waingiza bilioni 471

Mlima Kilimanjaro waingiza bilioni 471

Unknown | Tuesday, February 06, 2018 | 0 comments
Serikali imesema hifadhi ya Mlima wa Kilimanjaro katika kipindi cha miaka kumi kuanzia mwaka 2007 hadi 2017 imeingiza mapato ya Shilingi Bilioni 471 kupitia shughuli za utalii.

Mapato hayo yameelezwa jana Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga wakati akijibu swali la Mbunge wa Vunjo, James Mbatia aliyehoji mapato ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro na matumizi yake katika kipindi cha miaka kumi mfululizo.

Hasunga alitaja matumizi ya mapato hayo, kwamba kiasi cha Sh. Bilioni 67.5 zilitumika kutengeneza miundombinu ya kuhifadhi mlima na Bilioni 46.6 kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za hifadhi katika kipindi cha miaka kumi.

Pia, alisema Bilioni 2.28 zimetumika katika utekelezaji wa miradi ya kijamii kwenye vijiji vilivyo jirani na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG