Hoteli
ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam juzi ilitangaza ofa ya chumba cha
Sh22.4 milioni katika Usiku wa Valentine na kusema kuwa Watanzania
mbalimbali wamekuwa wakipiga simu kutaka kujua kama ni bei halisi na
wengine kuomba punguzo.
Hayo
yalisemwa na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Denis Glibic alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu
chumba hicho na namna watu walivyolipokea tangazo hilo.
Glibic
alisema tangu watangaze ofa hiyo ambayo ni kwa ajili ya wapendano
katika sikukuu ya Valentine, wamepokea simu nyingi kutoka kwa Watanzania
wakitaka kujua kama kweli hilo ni tangazo lao halisi na wengine
wakitaka wapate nafasi hiyo kwa punguzo la bei.
Kuhusu
chumba hicho ambacho kinatumiwa na marais mbalimbali duniani wanapokuja
nchini, meneja mwendeshaji wa hoteli hiyo, Timothy Mlay alisema, kwa
kawaida bei yake huwa ni Sh11.4 milioni kwa siku.
Alisema
pamoja na kuwapo kwa malalamiko ya maisha magumu, wanaamini watu
watapatikana kwani kwao kuanzia Desemba mpaka sasa ni kipindi ambacho
hupata wateja wengi.
Alisema
huduma zitakazotolewa kwa wateja wa chumba hicho siku hiyo zitakuwa
tofauti kwa wateja wengine, kwani mbali ya kwenda kuchukuliwa na gari la
kifahari eneo wanaloishi, pia watapatiwa zawadi za mapambo ya mwilini
yenye madini ya Tanzanite
0 comments:
Post a Comment