Mkutano
wa 10 wa Bunge umeanza leo Januari 30 mwaka 2018 mjini Dodoma kwa
wabunge wapya watatu wa CCM kula kiapo cha uaminifu mbele ya Naibu
Spika, Dk Tulia Ackson.
Wakati wabunge hao wakila kiapo, takribani wabunge 50 wa upinzani walikuwa nje ya ukumbi wa chombo hicho cha kutunga sheria.
Walioapishwa ni Dk Damas Ndumbaro (Songea Mjini), Justin Monko (Singida Kaskazini) na Dk Stephen Kisurwa wa Longido.
Pia,
Dk Tulia aliomba wabunge kusimama kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa
mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama ambaye alifariki dunia Novemba
mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment