Home » » LIVE UPDTES: Hali Ilivyo Kenya, 'Raila Odinga Akijiapisha Kuwa Rais'....Matangazo ya TV Yamezimwa

LIVE UPDTES: Hali Ilivyo Kenya, 'Raila Odinga Akijiapisha Kuwa Rais'....Matangazo ya TV Yamezimwa

Unknown | Tuesday, January 30, 2018 | 0 comments
Hali ya wasiwasi imetanda nchini Kenya baada ya kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Bwana Raila Odinga, kushikilia kuwa ataapishwa leo kama rais wa nchi hiyo.

Muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) umesema hafla hiyo itafanyika katika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi.

Baada ya sherehe hizo kuahirishwa mwezi uliopita, muungano mkuu wa upinzani nchini humo-NASA, bado unaendelea na msimamo wake wa kuwaapisha viongozi wake Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama Rais na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Kenya.

Maafisa wa polisi walifika asubuhi na mapema katika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi unaopanga kutumiwa na muungano wa Nasa kwa shughuli ya kumuapisha Bw Odinga.

Kituo cha habari cha kibinafsi cha Citizen kimeripoti kuwa maafisa wa polisi wameamrishwa kuondoka katika uwanja wa Uhuru Park.
==>Mabasi ya wafuasi wa upinzani yazuiwa Voi
Mabasi matatu yaliyokuwa yanawasafirisha wafuasi wa upinzani waliokuwa wanaelekea Nairobi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi wao Raila Odinga yamekamatwa na maafisa wa polisi katika mji wa Voi, katika barabara ya kutoka Mombasa kwenda Nairobi.

Mji wa Voi unapatikana takriban kilomita 330 mashariki mwa mji huo mkuu wa Kenya.

Afisa wa polisi amewaambia wanahabari kwamba madereva wa mabasi hayo walikuwa wamevunja sheria kadha za barabarani.

Wafuasi wa upinzani nchini Kenya wameanza kuingia uwanja wa Uhuru Park baada ya polisi kuondoka.Baadhi wanazunguka uwanja huo wakiimba ‘Uhuru Must Go’.
 
==>Wafuasi wa upinzani waliozuiliwa Voi waachiliwa
Wafuasi wa upinzani waliokuwa wanasafiri kuelekea Nairobi ambao walizuiliwa awali mjini Voi baadae wameachiliwa na kuruhusiwa kuendelea na safari.
==>Vituo vya habari vyafungiwa matangazo Kenya
Baadhi ya vituo vya redio na televisheni vya Royal Media Services (RMS), vikiwemo runinga ya Citizen TV, vimefungiwa matangazo pamoja na kituo cha televisheni cha NTV kinachomilikiwa na kampuni ya Nation Media Group (NMG) katika baadhi ya maeneo.

Vituo hivyo vimekuwa vikipeperusha matangazo kuhusu sherehe iliyopangiwa kufanyika leo ya kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga.

Serikali ilikuwa imetahadharisha vituo vya habari Kenya dhidi ya kupeperusha moja kwa moja hafla hiyo.

Mmoja wa wahariri wakuu wa Citizen Peter Opondo amesema  kwamba maafisa wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA)  wakiandamana na polisi walivamia vituo vya kupeperushia matangazo na kuzima matangazo.

Citizen TV ndicho kituo cha runinga kinachoongoza Kenya. Matangazo ya kituo cha NTV yanapatikana pekee kupitia ving’amuzi vya kulipia. Kituo kingine kikubwa KTN bado kinarusha matangazo.

==>Odinga: Kufungwa kwa vyombo vya habari inasikitisha
Raila Odinga amezungumza na vyombo vya habari dakika chache kabla ya kuelekea ‘kuapishwa’.

Akizngumza kwa njia ya simu na kituo cha habari cha KTN, Odinga amesema kuwa hawakutarajia kufungwa kwa vyombo vya habari.

Ni hali ya ‘kusikitisha’ na ‘inaonesha kuwa tumefika kiwango cha Uganda.'

Alielezea kuwa shughuli yao ni halali na haikiuki katiba. Pia amesema haamini kwamba wanachokifanya ni mapinduzi ya serikali.


Odinga: Tunachokifanya si mapinduzi ya serikali
Bw Raila Odinga amezungumza na kituo cha habari cha KTN kwa njia ya simu ambapo amesisitiza kwamba Rais Uhuru Kenyatta hakuchaguliwa kwa njia halali.

Alipoulizwa anni atamwapisha, amesema: "Ngoja uone” na akasisitiza kwamba wanachokifanya leo kina msingi wake katika sheria na si mapinduzi.

“Hatutambui uchaguzi wa Oktoba 26 (uchaguzi wa marudio ambao Odinga alisusia), zaidi ya asilimia 86 ya Wakenya hawakushiriki. Tuna serikali ambayo si halali ambao inajidai kuwa mamlakani,” amesema.

Kuhusu taarifa kwamba amepokonywa walinzi, amesema: "Walinzi wangu waliondolewa muda mrefu sana uliopita. Najihisi kuwa hatarini ndio lakini watu raia ndio usalama wangu.”

Bw Odinga ameitaka serikali kutotumia nguvu kuusambaratisha mkutano wa leo.

"Wafuasi wangu wamo safarini kuelekea Canaan. Safari yetu ni halisi na haiwezi kuzuiwa.
 


Odinga bado anasubiriwa Uhuru Park
Afisa mkuu mtendaji wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) Norman Magaya alikuwa amesema Bw Odinga, na viongozi wengine wa muungano huo wangewasili uwanjani katika muda wa dakika 40 hivi. Sasa hivi ni saa moja inaelekea kupita tangu wakati huo:

Credit: BBC

Advertisement
==
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG