Home » » Taarifa Mbaya kwa CHADEMA Kutoka Arusha

Taarifa Mbaya kwa CHADEMA Kutoka Arusha

Unknown | Monday, January 22, 2018 | 0 comments
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha kimepata pigo baada ya kumpoteza Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Karatu, Thomas Moshi Darabe ambaye amefariki Januari 21, 2018 ghafla wakati akipelekwa hospital

Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha juu ya kifo hicho na kusema kuwa familia ya marehemu leo itakaa na kupanga juu ya utaratibu wa mazishi wa kiongozi huyo.
"Ni kweli amefariki na leo familia itakaa na kupanga juu ya utaratibu wa mazishi kisha watatujuza, Thomas Moshi amefariki jana mchana na kifo chake kimetokea ghafla sana" alisema Mrema 
Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Karatu na diwani wa Kata ya Baray Mhe. Thomas Darabe amefariki jana wakati akikimbizwa Hospitali ya Selian Mkoani Arusha kupatiwa matibabu lakini umauti ulimkuta kabla ya kufika kwenye matibabu. 
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE APUMZIKE KWA AMANI.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG