Mkuu wa shule ya sekondari
ISAPULANO Mwl. METHOD SANGA shule iliyoko wilayani Makete mkoani Njombe ameeleza kuridhishwa na
mapokezi ya wananchi wa kata ya Isapulano hususani wananchi wa kijiji cha Isapulano
kwa ushirikiano walio toa tangu kuanza Rasmi kwa shule hiyo Januali 8 mwaka
huu.
Mwl Sanga amesema shule ya
sekondari ISAPULANO yenye namba za usajili
S1050 nishule ya mkondo mmoja inajumla ya wanafunzi 39 wakiwemo wavulana
22 na wasichana 17 imeanza rasmi Januari 8 2018 ikiwa na walimu watatu huku
mazingira ya kujifunzia yakiwa rafiki kwa wanafunzi na walim hasa katika upande
wa miundombinu.
Aidha mkuu huyo amewashukuru
wadau wa elimu ikiwemo Halmashauri ya wilaya Mbunge wa jimbo la Makete Prof
Norman Adamson Sigara king,Diwani wa kata ya Isapulano wa fanyabiashara wa ndani
na nje ya isapulano pamoja na wananchi wa kijiji cha Isapulano kwa usirikiano walio utoa hadi kufanikisha
shule kupata usajili na kuanza rasmi .
Mwl CHIKU MDINDILE ni miongoni
mwa walimu wanaofundisha shule ya sekondari Isapulano amesema wamejipanga
kuhakikisha shule hiyo inapata sifa nzuri kwa kufanya vizuri kitaaluma kwakuwa
ipo katika mazingira mazuri na wananchi wamehamasika katika kuijenga shule yao
huku wakitoa ushirikiano mkubwa hasa katika mambo yakijamii.
Wakizungumzia baadhi ya
changamoto wanazokumbananazo walimu wa shule ya sekondari Isapulano wamesema
nyumba za walimu maabara pamoja na baadhi ya vitendea kazi hasa kwa upende wa
vitabu na vifaa vya maabara kwasasa
nivichache ambapo ameomba wadau wa elimu kuendelea kujitolea kwaajiliya
kutatua changamoto hizo muda mufupi kabla ya kuaanza silabasi.
Baadhi ya wanafunzi wametoa
wito kwa jamii na serkali kwa ujumla kuendelea kujenga shule hiyo ili kutengeneza
mazingira rafiki kwao pamoja na walimu huku wakieeleza kufurahishwa na uwepo wa
shule hiyo kwakuwa imewapunguzia Gharama na muda wakufuata mahitaji makwao ambapo hapo awali walishuhudia ndugu
zao wakiwapeleka watoto wao shule za mbali na kushindwa kumudu huduma muhimu
kwa wanafunzi.
Pamoja na jitihada za
wananchi wa kijiji cha isapulano kujenga shule nzuri likini miundombinu ya
barabara kwao imekuwa tatizo hivyo wananchi hao wameomba serkali pamoja na
wadau wengine kufukia sehem korofi katika barabara ya makete kupitia vijiji vya
luvulunge na Isapulano kwenda Mbeya ili kurahisisha mawasiliano ya barabara kwa
wanafunzi na jamii nzima kwa ujumla.
hii ni sahem mojawapo korofi katika barab ara ya Isapulano.
0 comments:
Post a Comment