Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Ahazi Ndelwa Lusemba (Y-Jay) kutoka Makete
Mkoani Njombe ameelezea mazingira kuwa kikwazo cha wasanii wa mikoani
kuweza kuendana na kasi ya soko la muziki na ushindani mkubwa uliopo kwa
sasa.
Y-Jay ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na AFRICAN NEWS BLOG wakati
alipotakiwa kueleza sababu za kutoachia kazi kwa kasi kulingana na
ushindani uliopo,
Aidha
kutokana na mazingira kutokuwa na fulsa kimuziki na kutumia gharama
kubwa kutafuta soko la muziki na kufanya promotion kwake na wasanii wa
mikoani amewaasa wasanii kufanya maandalizi kabla ya kuingia kwenye soko
la ushindani.
Hata hivyo kwa mwaka 2018 amesema kwa siku zijazo anatarajia kuachia kazi mpya itakayo kwenda kwa jina la NITULIE,
Y
- JAY Ni miongoni mwa wasanii kutoka Mkoani Njombe ambaye kwasasa
anafanya vizuri na nyimbo tatu , pigo la moyo,fadhira na Show Love
amewataka wadau wa muziki kutambua umuhim wa sanaa na kusaport kazi za
wasanii wa Mikoani.
<ihttps://youtu.be/tyfIvfZ68Ps
0 comments:
Post a Comment