Tazama Hapa Ratiba Nzima na Makundi Yote ya Kagame Cup 2018

Unknown | Tuesday, June 05, 2018 | 0 comments
Wakongwe wa soka Tanzania, Simba SC na Yanga SC wamepangwa Kundi C katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame Cup inayotarajiwa kuanza Juni 28 hadi Julai 13 mwaka huu mjini Dar es Salaam.
 
Akitaja makundi ya michuano hiyo, Katibu wa kudumu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye alisema kwamba pamoja na Simba na Yanga, timu nyingine katika Kundi hilo ni Dakadaha ya Somalia na Saint George ya Ethiopia.
 
Musonye alisema kwamba Kundi A linaundwa na timu za Azam FC, KCCA ya Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC wa Sudan Kusini, wakati Kundi B linaundwa na timu za Rayon Sport ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djibouti. Musonye aliishukuru Tanzania kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo na akasema kwamba anatarajia itafana kwa sababu ya rekodi ya nchi hii kuandaa mashindano yaliyokuwa na msisimko mkubwa miaka ya nyuma.
 
Musonye ambaye alisema mashindano yatafanyika viwanja vya Taifa na Azam Complex, Chamazi – pia amewapongeza Rwanda na Rais wao, Paul Kagame kwa kuwa wadhamini wa mashindano haya kwa zaidi ya miongo miwili sasa.
 
Musonye amesema kwamba wamelazimika kufanya mashindano ya mwaka huu sambamba na Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi, kwa sababu wasipofanya mwezi huu hayatafanyika tena kwa mwaka wa tatu mfululizo. 
 
Hata hivyo, Musonye amesema kwamba watatoa ratiba nzuri ambayo haitaruhusu mashindano ya mwaka huu kuingiliana na mechi za Kombe la Dunia.  
 
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Tido Mhando alisema kwamba wataitumia michuano hiyo kukizindua kituo chao chao Redio, Uhai FM na akawahakikishia kwamba pamoja na mashindano hayo kufanyika sambamba na Kombe la Dunia, lakini yatafana 
 
FIFA imeridhia Kagame kufanyika mwezi huu tofauti na agizo lake la kutotaka katika mwezi wa Fainali za Kombe la Dunia yasifanyike mashindano mengine yoyote, kwa sababu washiriki watano wa michuano hiyo wapo kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Afrika, ambayo kwa sasa imesimama kupisha Kombe la Dunia itarejea Julai baada ya kumalizika kwa michuano hiyo nchini Urusi.
 
Hao ni KCCA ya Uganda iliyopo Kundi A katika Ligi ya Mabingwa Afrika na nyingine nne kwenye Kombe la Shirikisho ambazo ni Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sports ya Rwanda, Yanga ya Tanzania zilizopoi Kundi D zote na Al-Hilal ya Sudan iliyopo Kundi A.
 
Na kwa sababu hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Afrika itakwenda hadi Agosti, mwezi ambao msimu mpya wa Ligi Kuu nyingi duniani huanza – michuano ya Kagame isipofanyika mwezi huu kuna hatari isifanyike tena na mwaka huu kwa mara ya tatu mfululizo.
 
Azam FC ndiyo mabingwa wa mwisho wa michuano hiyo ilipofanyika Tanzania, walipowafunga Gor Mahia 2-0 katika fainali Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, mabao ya waliokuwa washambuliaji wake hatari, John Raphael Bocco dakika ya 17 na Muivory Coast, Kipre Herman Tchetche dakika ya 64.
 
Na hiyo ndiyo ilikuwa michuano iliyomtoa mshambuliaji Mkenya, Michael Olunga ambaye kwa sasa anachezea Girona FC ya Hispania kwa mkopo kutoka Guizhou Zhicheng ya China.
 
Baada ya kufungha mabao matano akiwa na Gor Mahia na kuibuka mfungaji bora akiwapiku , Osman Bilal Salaheldin wa Al-Khartoum ya Sudan aliyefunga mabao manne sawa na Tchetche wa Azam FC, Olunga akachukuliwa na Djurgardens IF ya Sweden mwaka 2016 iliyomuuza Guizhou Zhicheng mwaka 2017.
 
Na Tanzania itawakilishwa na Azam FC kama mabingwa watetezi wa mashindano na Yanga SC, kama mabingwa wa nchi.

Credit: Full Shangwe 

Advertisement

Waziri Ataka Watoto Walioungana Kagera Wafikishwe Muhimbili Haraka

Unknown | Tuesday, June 05, 2018 | 0 comments
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Ummy Mwalimu amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, kuhakikisha watoto waliozaliwa wakiwa wameungana wanafikishwa Muhimbili.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo ambaye alihoji je serikali ina taarifa kuwa kuna watoto wamezaliwa Kagera wakiwa wameungana.

Akijibu swali hilo, Ummy amesema: “Wanaozaliwa wakiwa na maumbile ya ajabu wapelekwe hospitali.

“Na kuhusu watoto waliozaliwa wakiwa wameungana huko Kagera, namwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera ahakikishe watoto hao wanafikishwa Muhimbili,”.

Advertisement

Spika Ndugai ‘ampokonya’ mwenyekiti uongozi baada ya wapinzani kuitwa mbwa

Unknown | Tuesday, June 05, 2018 | 0 comments

Spika Job Ndugai leo amelazimika kumpokonya Najma Giga uongozi wa kikao cha Bunge baada ya mzozo uliosababishwa na mbunge wa CCM aliyewafananisha wapinzani na mbwa.

Spika Ndugai alifanya kitendo hicho kisicho cha kawaida katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya mwaka 2018/19 ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Wakati akichangia, mbunge huyo wa Jang’ombe, Ali Omar alisema: “Ukiona majuha wanapongezana wakaona wamefanya la maana, kuna hawa mbwa kama tutawatoa itakuwa vizuri sana. Nasikia milio ya mbwa ukiwatoa itakuwa vizuri.”

Baada ya kauli hiyo, wabunge wawili kutoka Chadema, Joseph Selasini (Rombo) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) walisimama kutaka utaratibu ufuatwe kwa mchangiaji kuomba radhi.

Hata hivyo, Giga hakuruhusu hilo na kusababisha wabunge wengine wa upinzani kupiga kelele wakimtaka mbunge huyo afute kauli hiyo.

Giga alitumia kama dakika mbili kuwazuia lakini hakuweza na kumtaka Omar aendelee kuchangia.

Hata hivyo hakuweza kuwazuia kutokana na wabunge hao wa upinzani kuendelea kupiga kelele wakisisitiza Omar ashinikizwe kufuta kauli yake.

Wakati kelele zikiendelea na utulivu bungeni ukitoweka, Spika Ndugai akaingia na kuchukua uongozi wa kikao na hivyo Giga, aliyeanza kuongoza kikao hicho tangu asubuhi, kulazimika kumuachia uongozi.

Credit: Mwananchi

Advertisement

Spika Ndugai ‘ampokonya’ mwenyekiti uongozi baada ya wapinzani kuitwa mbwa

Unknown | Tuesday, June 05, 2018 | 0 comments
Spika Job Ndugai leo amelazimika kumpokonya Najma Giga uongozi wa kikao cha Bunge baada ya mzozo uliosababishwa na mbunge wa CCM aliyewafananisha wapinzani na mbwa.

Spika Ndugai alifanya kitendo hicho kisicho cha kawaida katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya mwaka 2018/19 ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Wakati akichangia, mbunge huyo wa Jang’ombe, Ali Omar alisema: “Ukiona majuha wanapongezana wakaona wamefanya la maana, kuna hawa mbwa kama tutawatoa itakuwa vizuri sana. Nasikia milio ya mbwa ukiwatoa itakuwa vizuri.”

Baada ya kauli hiyo, wabunge wawili kutoka Chadema, Joseph Selasini (Rombo) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) walisimama kutaka utaratibu ufuatwe kwa mchangiaji kuomba radhi.

Hata hivyo, Giga hakuruhusu hilo na kusababisha wabunge wengine wa upinzani kupiga kelele wakimtaka mbunge huyo afute kauli hiyo.

Giga alitumia kama dakika mbili kuwazuia lakini hakuweza na kumtaka Omar aendelee kuchangia.

Hata hivyo hakuweza kuwazuia kutokana na wabunge hao wa upinzani kuendelea kupiga kelele wakisisitiza Omar ashinikizwe kufuta kauli yake.

Wakati kelele zikiendelea na utulivu bungeni ukitoweka, Spika Ndugai akaingia na kuchukua uongozi wa kikao na hivyo Giga, aliyeanza kuongoza kikao hicho tangu asubuhi, kulazimika kumuachia uongozi.

Credit: Mwananchi

Advertisement

Mbunge CUF ataka Maalim Seif ahojiwe TAKUKURU

Unknown | Tuesday, June 05, 2018 | 0 comments
Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Ally amelitaka Bunge kuamuru, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ahojiwe na Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kutopeleka hesabu za fedha za chama kukaguliwa na CAG.

Khatib alitoa kauli hiyo leo bungeni wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2018/19.

“Hapa wote tumeng’ang’ania kwenye Sh trilioni 1.5 lakini mimi nataka zile Sh bilioni 200 zije Zanzibar. Leo nitakuwa tofauti kwa sababu nitapataje ujasiri wa kuhoji 1.5 trilioni wakati hesabu fedha za chama changu hazijapelekwa kwa CAG kukaguliwa?” amehoji.

Kutokana na hilo, amesema Katibu Mkuu wa Chama chake hajakitendea haki chama kwa kutopeleka mahesabu kwa CAG.

“Katibu Mkuu wangu ahojiwe na Takukuru kwanini hakupeleka hesabu za fedha zikaguliwe? Haya mambo yanataka ujasiri sana.

“Mheshimiwa Spika naomba kanuni inayomlinda mbunge inilinde maana isije ikaja kama ilivyowakuta wenzangu,” amesema.

Kutokana na hilo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amemwmabia mbunge huyo kuwa katika jambo hilo wanamuunga mkono kwa kuwa ni la maana.

Advertisement

Waziri Mkuu Ampongeza Steven Masele

Unknown | Tuesday, June 05, 2018 | 0 comments
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika Mheshimiwa Stephen Masele na kumuahidi kwamba Serikali itampa ushirikiano ili aweze kutimiza majukumu yake.

Ametoa ahadi hiyo leo (Jumanne, Juni 5, 2018) wakati akizungumza na Mheshimiwa Masele ofisini kwake Bungeni, Dodoma. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza kwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo.

Amesema ushindi wake katika nafasi hiyo umelipa heshima kubwa Bunge na Serikali na kwamba wana matarajio makubwa kwa sababu uwepo wake, utaliongezea Taifa ushirikiano na nchi nyingine za Afrika.

"Matarajio kwa Bunge ni makubwa kwani kuna mambo ambayo tunataka ushirikiano na nchi nyingine za Afrika, hivyo uwepo wako ni muhimu katika kufanikisha utekelezaji wake."

Vilevile, Waziri Mkuu amewapongeza wabunge wengine wawili, Waheshimiwa David Silinde na Asha Abdullah Juma kwa ushirikiano wao uliochangia ushindi wa Mheshimiwa Masele.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Masele ambaye ni Mbunge wa Shinyanga Mjini, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyompa na hatimaye kuibuka na ushindi huo.

Amesema ushindani ulikuwa mkali kutokana na uwepo wa mataifa mengi yaliyokuwa yakiwania nafasi hiyo. Aliahidi kutetea maslahi ya Taifa kwa muda wote atakaotumikia nafasi hiyo. “Nakuhakikishia Waziri Mkuu kwamba nitayalinda na kuyatetea maslahi ya Tanzania kwa muda wote ambao nitakuwa katika wadhifa huu,” alisema Mhe. Masele.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Advertisement

Wabunge Wahoji Ahadi ya Milioni 50 Kwa Kila Kijiji Iliyotolewa Na Rais Magufuli

Unknown | Tuesday, June 05, 2018 | 0 comments
Ahadi ya Chama Cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 ya kutoa Sh. milioni 50 kwa kila kijiji na kila mtaa kwa sehemu za mijini, ambayo haijatekelezwa kwa miaka miwili mfululizo huenda ikaanza kutekelezwa baada ya jana Bunge kuitaka serikali kutoa taarifa bungeni kuhusu utekelezaji wake.

Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma jana taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu makadirio ya bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka ujao wa fedha, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Jitu Soni, alisema pamoja na kwamba serikali iliahidi kutoa Sh. milioni 50 kwa kila kijiji, hadi sasa hakuna fedha yoyote iliyotolewa.

Alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17, serikali ilitenga Sh. bilioni 60 (Fungu 21) na katika mwaka huu wa fedha ilitenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kufanya utafiti wa majaribio kwa baadhi ya mitaa, vijiji, kata na shehia kutekeleza mradi huo.

"Hata hivyo, fedha hizo zilizotengwa katika miaka yote, hakuna fedha yoyote iliyotolewa licha ya serikali kuahidi na kuweka utaratibu maalum kuhusu utoaji wa Sh. milioni 50 kwa kila kijiji kupitia Tamisemi," alisema.

"Kamati ingependa Bunge lako tukufu lipewe taarifa ya utekelezaji wa mradi huu ikiwamo 'Pilot Study' (utafiti wa majaribio) iliyofanyika," alisema.

Kiongozi huyo wa kamati pia alisema tathmini ya jumla ya mwenendo wa utoaji wa fedha za utekelezaji bajeti ya mwaka 2017/18 si wa kuridhisha kwa baadhi ya mafungu.

"Hadi kufikia Machi, mwaka huu, kati ya mafungu nane yaliyo chini ya wizara, ni miwili tu yaliyokuwa yamepokea fedha zaidi ya asilimia 60 ya bajeti zilizoidhinishwa na Bunge," alisema na kueleza zaidi:

"Kati ya mafungu 47 ya wizara mbalimbali yanayostahili kupata fedha za maendeleo ni mafungu 16 tu yamepata fedha zaidi ya asilimia 50."

Pia alisema mapato yatokanayo na ushuru wa usafirishaji wa fedha na bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa kama pombe kali yameshuka kwa asilimia 30.

"Kamati inaendelea kuishauri serikali kuhakikisha kwamba sera zake za kikodi kwa sekta zinazokua ziwe zina lengo la kulea na kuendeleza sekta hizo na si kukusanya kodi kiasi ambacho kinaathiri hata ukuaji wa sekta husika,"alisema.

Jitu pia alisema pamoja na michezo ya kubahatisha kukua kwa kasi na kuipatia serikali mapato, kamati yake inashauri kupanda kwa ada, tozo na kodi mbalimbali kwa kuwa kimsingi michezo hiyo si ya kiuzalishaji na imekuwa na madhara makubwa kwa jamii.

"Katika nchi za Afrika Mashariki, Tanzania inaongoza kwa kutoza kiwango cha chini kwenye mapato ghafi ya michezo ya kubahatisha kuliko nchi nyingine," alisema.

Alitolea mfano Kenya kuwa inatoza asilimia 35, Rwanda asilimia 13 na Uganda inatoza asilimia 20 ya mapato ghafi.

Alisema kamati inaitaka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT) kusimamia kikamilifu sheria ili kuhakikisha kwamba wanaoshiriki katika michezo hiyo wawe wanafikia umri wa miaka 18.

Jitu pia alisema kamati yake inaishauri serikali kuhakikisha inalipa madeni yote ya watumishi, makandarasi na wazabuni yaliyohakikiwa.

Advertisement

Polisi Shinyanga Wakamata Silaha Za Kivita,waua Majambazi Wanne Makaburini Kahama

Unknown | Tuesday, June 05, 2018 | 0 comments

Na Kadama Malunde
Watu wanne wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi eneo la makaburi  ya Kitwana kata ya Busoka tarafa ya Kahama Mjini wilayani Kahama wakati wakijaribu kuwatoroka askari waliokuwa kwenye msako mkali wa kuwatafuta majambazi wanaojihusisha na matukio ya uhalifu katika wilaya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makaburi ya Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama jana Jumatatu Juni 4,2018,Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule alisema tukio hilo limetokea Juni 3,2018 majira ya saa sita na dakika 40 mchana.

Amewataja waliouawa kuwa ni Minani Deo (33) mkazi wa Mabanda Burundi ambaye pia ni muagizaji wa silaha haramu kutoka nchi jirani na Masalamali Paulo (34) mkazi wa Geita ambaye aliachiwa kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt. John Pombe Magufuli katika gereza la Butimba mkoani Mwanza mwezi Aprili 2018.

Wengine waliouawa ni Hussein Issa Jumanne maarufu kwa jina la Shehe (30) mkazi wa Nyasubi Kahama,Maduhuli Cheyo Maselegu (42) mkazi wa Kigoma Ujiji.

Akielezea zaidi kuhusu tukio hilo,Kamanda Haule alisema siku ya tukio watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa risasi sehemu mbalimbali za miili yao na kufariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali ya Mji wa Kahama.

“Walikuwa wanaelekea kuwaonyesha askari polisi bastola na bomu moja la kutupwa kwa mkono ‘Hand Grenade) pamoja na washirika wenzao wa ujambazi,wakiwa tayari wameonesha bastola na bomu hilo lililokuwa limechimbiwa chini ya ardhi ndipo walipotaka kuwakimbia askari na askari wakawafyatulia risasi”,alifafanua Kamanda Haule.

“Chanzo cha tukio hilo ni kutaka kuwatoroka askari waliokuwa kwenye msako mkali wa kuwatafuta majambazi wanaojihusisha na matukio ya uhalifu hasa katika wilaya ya Kahama kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2018”,aliongeza.

Aidha alisema takwimu zinaonesha majambazi hao walikimbilia mkoani Tabora na mara baada ya askari kufika mkoani Tabora wakapata taarifa kuwa majambazi hao wamekimbilia mkoani Kigoma na polisi kufanikiwa kumkamata Masalamali Paulo eneo la soko la Mwanga mkoani Kigoma.

“Baada ya kumkamata na kumhoji aliwataja washirika wenzake watatu wa ujambazi ambao walikimbilia Katumba mkoani Katavi na kufanikiwa kuwakamata wakiwa na silaha ya kivita aina ya AK47 yenye namba UA-2651-1997 iliyokuwa na risasi 30 ndani ya magazine moja ambayo ilipatikana karibu na uwanja wa ndege mkoani Katavi”,alieleza.

Aliongeza kuwa silaha hiyo pia ilikuwa imehifadhiwa pamoja na bastola moja aina ya Browning yenye namba 17569465 ikiwa na risasi 15 ndani ya magazine yake ndani ya shimo.

Alisema katika mahojiano na majambazi hao walikiri kufanya matukio ya uhalifu katika wilaya ya Kahama na mikoa ya Tabora,Geita,Morogoro,Kigoma na Katavi na kwamba miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Mji wa Kahama.

Wakati huo huo,Kamanda Haule alisema mnamo tarehe 28.5.2018 majira ya saa moja na nusu usiku katika mtaa na kata ya Mhungula wilayani Kahama ikipatikana silaha moja aina ya shortgun yenye namba B-15939 iliyokuwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa imehifadhiwa kwenye mfuko wa sulphate ndani ya nyumba ya Malale Kalikisu Malale aliyekuwa anatafutwa na polisi kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Alisema mtuhumiwa alikimbia kabla ya kukamatwa na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea.

Kamanda Haule amewataka wahalifu wote kujisalimisha pamoja na silaha zao ndani ya mkoa au nje ya mkoa na wasipofanya hivyo wataendelea kuwafuatilia sehemu yoyote waliyojificha iwe chini ya ardhi,angani au ziwani ili wachukuliwe hatua za kisheria.

“Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli kwa mapenzi yake na wananchi wake,kwa huruma yake aliamua kuwaachia huru wahalifu waliokuwa wamefungwa gerezani akiwemo huyu Masalamali Paulo warudi uraiani,wajirekebishe na washiriki kwenye shughuli za uchumi,sasa baadhi ya hao wahalifu wanauchukulia huu msamaha katika njia ambazo siyo sahihi,hivyo wote walioachiwa kwa msamaha wa rais waendane na maadili mema katika jamii”,alieleza.

“Ndugu wananchi naomba turejee kauli ambayo inatolewa mara kwa mara na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Nyakoro Sirro kuwa uhalifu haulipi, uhalifu hauna nafasi nami pia naungana na kauli ya afande IGP kurudia maneno hayo hayo kuwa kwa sasa uhalifu mkoani Shinyanga hauna nafasi,tunataka wananchi wafurahie matunda ya uhuru,matunda ya uhuru ni amani na utulivu",

"Wananchi wafanye shughuli zao za kiuchumi bila ya kuwa na hofu yoyote ile ya matishio ya kiusalama ili kusudio la kuleta maendeleo katika jamii litimie,natoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili ziweze kufanyiwa kazi mapema”,alisema.
  
Credit :Malunde


Advertisement

Mti Mweupe Wa Kuona Wachawi Na Ulozi Katika Mapenzi.

Unknown | Tuesday, June 05, 2018 | 2comments
Kuna mti mmoja (jina lake linahifadhiwa ) unapatikana porini, mti huo ukikomaa, urefu wake hauzidi wa mtoto wa miaka saba, una magamba kwa mbali na rangi yake ni nyeupe

Mti huu ukikauka ukausaga unga wake huwa mweupe kama mti wenyewe.

Ukichukua unga wa mti huu halafu ukajipaka usoni unakuwa na uwezo wa kuwaona wachawi  na  misukule.

Ukijipaka unga wa mti huu usoni halafu ukatembea mtaani wakati wa mchana, unaweza kuona mambo yote yanayofanyika katika siri kubwa kama vile wachawi wakiwa wanawanga au wanafanya shughuli zao wakiwa uchi.

Mti huu unakufanya  pia  kuwa  na  uwezo  wa  kuwaona  misukule  na  kama  wewe  ni  mfanyabiashara ya  duka  basi  mti  huu  utakupa  uwezo  wa  kuwaona  watu  wanao  kuja  dukani kwako  na  hela  za  chuma  ulete.

Vilevile mti huu una uwezo wa kukimbiza nyoka mfano ukiwa na kipande cha mti huu mfukoni halafu ukawa unatembea, kama mbele yako kuna nyoka atakimbia kabla hujafika.

Pia  mti  huu hutumiwa  na  watu  wanao  fanya  shughuli ya  kutafuta  mali  zenye  asili  ya  kukaliwa, kushikiliwa,kulindwa  na  kufichwa  na  majini  wa  kisheitwani  kama  vile  madini  na  mali  mbalimbali.

Kwa ufupi  mti  huu  unakaliwa  na  majini ambao  kazi  yao  kuu  ni kufunua  mambo  yaliyowekwa  sirini  na  kufichua  mambo  yote  yaliyofichwa.

Kwa  hiyo  mtu  akichanjiwa  ama  kupakwa  uchawi  huu  anakuwa  na  uwezo  wa  kuona  mambo  yaliyo  fichwa na  kuwekwa  sirini.

MTI  MWEUPE  WA  KUONA  WACHAWI NA  ULOZI  KATIKA MAPENZI.
Mti mweupe  una  matumizi mengi  sana. Moja  kati  ya  matumizi  hayo  ni  pamoja  na  kutumika  katika  ulozi  wa  mapenzi.

Katika  ulozi  wa  mapenzi, mti  mweupe  hutumika  Zaidi  katika  uchawi  wa  mapenzi  ambao  hutupwa  kwa  njia  ya  kumtegea  mtu  kwenye  njia  anayo  itumia  kupita.

Kama  unataka  kumtega  mtu  ulozi  wa  mapenzi, basi  usiku  utachukua  huu  mti  mweupe  kiasi  utajipaka usoni, kiasi  utaufunga  kwenye  kitambaa  chekundu  na  kuweka  chini  ya  mto  ambao utaulalia  na  kiasi  utachoma  kwenye  koroboi  au  chetezo  huku  ukimnuizia  mtu  ulie  mkusudia  na  kuwaomba  majini  wanao husiana  na  mti  huu mweupe  wakufunulie  na  kukuonyesha  njia  ambayo  mtu  ulie  mkusudia  atapita kesho  yake  au  katika  siku  maalumu  ya  kinyota  ambayo  umepanga  kumtega  mtu  huyo  uchawi  huo  wa  mapenzi.

Usiku  wa  siku  hiyo utamuona  katika  ndoto  mtu  ulie mkusudia  akipita  katika  njia  ambayo  wewe unaifahamu.

Ikifika  kesho  yake  asubuhi  utatakiwa  kwenda  katika  njia  hiyo  na  kutega  dawa  nyingine  ya  ulozi  wa  mapenzi  ambayo  hutumika  kwa  kumtega  mtu  aruke ili  imnase. 

Na  mtu  huyo  akisharuka  katika  njia  hiyo  basi  dawa itamnasa  na  jinni wa  mapenzi  aliekusudiwa  atamuingia  mtu  huyo  na  kuamuru  kufanya  mambo  yote  ambayo mlogaji  alikusudia  kuyafanya.

Hivyo  ndivyo  mti  mweupe  wa  kuona  wachawi  unavyo  tumika  katika  ulozi  wa  mapenzi.

Mbali  na  kutumika  katika  ulozi  wa  mapenzi  mti  huu  unatumika  katika  mambo  mengine  mengi  sana  mazuri  kwa  mabaya.

Mambo  yote  hayo  utayapata  kuyafahamu  kupitia  kitabu  changu  ambacho  kitatoka  mwezi  wa  saba  kati  kati. Kitabu  hicho  kinaitwa : MAMBO  TISA  YANAYO  UNDA  NYOTA YA  MWANADAMU NA  UHUSIANO  KATI  YA  NYOTA  YA  MTU  NA  MAFANIKIO YAKE  KATIKA  MAISHA  ambacho  kimeandikwa  nami  DOKTA. MUNGWA  KABILI.

Ndani  ya  kitabu  hiki  utapata  kufahamu  kila  kitu kuhusu  mti mweupe, kuanzia  taratibu  za  kuuchukua  porini, siku  na  muda  unao  takiwa  kuuchukua  porini, maneno  unayo  takiwa  kuyatamka wakati  unauchukua  mti  huu  porini, masharti  ya  kutumia  mti  huu, jinsi  unavyo  weza  kujiepusha  na  shari  za  wachawi  na  walozi  zitokanazo  na  kuutumia  mti  huu  pamoja  na  matumizi  yote  ya  mti  huu  kuanzia  kujipaka, kuchanjiwa,kuchoma, kufukiza, kupuliza  pamoja  na  mambo  yoote  yanayo  husiana  na  mti  huu.


MAKALA  HAYA  YAMEANDALIWA  NA  DOKTA. MUNGWA  KABILI.  ANAPATIKANA KWA  SIMU  NAMBA  0744  000 473.

Advertisement

Kijana Wa Saudia Ashinda Dola 5,000 Tuzo Ya Kimataifa Ya Kuhifadhi Quran

Unknown | Monday, June 04, 2018 | 0 comments
KIJANA wa miaka 18 kutoka Saudi Arabia, Ibn Rayizah Hatim Abdullah ameibuka na kitita cha dola za Marekani 5,000 kwenye fainali za 26 za tuzo ya Kimataifa ya Quran tukufu.

Kijana Rayizah ameibuka na kitita hicho baada ya kuwashinda wenzake sita waliofanikiwa kuingia fainali hizo ambao walitoka Yemen, Zanzibar, Malaysia, Mali, Marekani na Tanzania Bara.

Nafasi ya pili imechukuliwa na kijana Hamza Soukouna (25) kutoka Mali ambaye amejishindia dola za Marekani 4,000 na ya tatu imechukuliwa na Hamza El-Habashiy (18) kutoka Marekani ambaye amejishindia dola za Marekani 3,000. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania, mwaka huu yalishirikisha vijana 16 kutoka nchi 16 duniani.

Akizungumza na mamia ya waumini wa Kiislamu waliofurika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo mchana (Jumapili, Juni 3, 2018), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini hiyo waendelee kuwakamata vema vijana waliohifadhi Quran na kuwaendeleza kitaaluma katika fani nyingine za elimu ya kimazingira.

“Leo hii nimefarijika sana kusikia kwamba tunao vijana wetu ambao si tu wamehifadhi Quran bali pia wamehitimu fani mbalimbali katika elimu ya juu. Uwepo wa vijana wa namna hii ni muhimu katika kujenga jamii bora na yenye kuzingatia uadilifu katika kutekeleza majukumu yao,” amesema.

Amesema kazi ya kuhifadhisha Quran haiishii katika kujua kuisoma pekee. “Kuhifadhisha Quran kunapaswa kuwa msingi imara katika kujenga jamii bora kupitia mafunzo sahihi ya tabia njema, utii lakini pia kujua mipaka katika maisha yetu ya kila siku. Kwa kufanya hivyo, tutawasaidia vijana hawa tunaowahifadhisha Quran kuwa raia wema, wazalendo, wanaotambua  wajibu wao, majukumu yao, kwao wenyewe na kwa nchi yao pia,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wanaoendesha taasisi za kuhifadhi Quran wakae pamoja na watengeneze ratiba ya mashindano ya kitaifa na kimataifa ili waweze kuwa na mashindano yanayoanzia ngazi za chini hadi za juu.

“Kaeni pamoja, mtenge ratiba ya kuanzia ngazi ya kimataifa hadi kimataifa, ratiba hizi zipangwe na kutambulika kitaifa. Wekeni ratiba ili washiriki washindane kuanzia mikoani, ushindani uwepo na tuwaone wakipanda kutoka mkoa, Taifa, Afrika Mashariki, Afrika hadi ya Dunia,” amesema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira hiyo, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali alisema wameanza kuona matunda ya kazi ya kuhifadhisha Quran kwani vijana wa Kitanzania wamesoma elimu ya mazingira (circular education) na elimu ya dini na wamefaulu vizuri sana.

“Sasa hivi tunataka watoto wetu wafikie elimu ya juu ya dini na hii ya mazingira. Tunawapongeza hawa vijana wa Kitanzania ambao walienda hadi nje ya nchi kutafuta elimu ya juu na sasa wamerudi nyumbani kuasaidia ndugu zao,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania, Sheikh Othman Ali Kaporo alisema jumuiya ilianza kazi zake kimyakimya mwaka 1984 lakini ilianza kujulikana mwaka 1992

Alisema walianzisha jumuiya kwa sababu walibaini kuwa jamii ina kiu ya kupata watu wema watakaochangia maendeleo wa Taifa. “Ukiangalia mwelekeo wa vijana wetu wa Kiislamu si mzuri. Hebu fanya utafiti wa kina wa wale waliokuwemo magerezani. Je tunaumizwa na jambo hili? Na kama tunaumizwa tunafanya nini ili kuwaokoa vijana hawa? Haya ndiyo tunayalenga sisi, na kwa kupitia Quran, tuweze kuwaokoa na majanga yale,” alisema.

“Kuna vijana wengi wana vipaji lakini vinakufa kwa sababu hakuna wa kuviendeleza vipaji vyao. Kupitia Quran tukufu, tunahitaji kuwabadilisha wote hawa ili tuwe na jamii imara, inayomjua Mwenyezi Mungu, iliyobora na inayoishi kwa amani,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG