Shirikala la umoja wa mataifa linalo shughurika na Elimu ,sayansi na Utamaduni (UNESCO)
imeendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka katika Redio za
jamii nchini juu yaTathimini na ufuatiliaji (Monitoring and Evaluation) lengo likiwa ni kuibua na kutafutia ufumbuzi changamoto zinazo
ikabili jamii ya kitanzania kupitia vipindi na habari zenye kuleta
matokeo chanya .
Mwezeshaji kutoka UNESCO Bw,MARCO GIDEON
ametoa wito kwa washiriki kufanya kazi kwa kufuata kanuni , miongozo na maadili katia taaluma ya habari ili kuendana na malengo ya milenia hadi ifikapo mwaka 2030 ambapo amesema shirika limelenga kujengea uwezo Redio za jamii ili kuibua na
kutafutia ufumbuzi wa changamoto zinazo ikabili jamii.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya tathimini na ufuatiliaji (M&E )kutoka redio mbalimbali wameishukuru
UNESCO kwa mafunzo wanayoyatoa kwa redio za Jamii huku wakiomba shirika
kuendelea na miradi ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kuleta
mabadiliko chanya kwa jamii.
Revocutus
Msafiri ni miongoni mwa washiriki wa semina hiyo amesema mafunzo yanayotolewa na UNESCO yameleta matokeo kwa redio za jamii ikiwemo waandishi wa habari kupata uzoefu katika uandaaji na ufanyaji wa vipindi na habari huku akitoa rai kwa vyombo vingine pamoja na wadau wa
habari kushirikiana katika kubuni miradi itakayo ibua changamoto na kuzitafutia majibu yatakayopelekea kuibadilisha jamii pamoja na kuleta maendeleo.
Aidha mafunzo hayo yametolewa na shirika la UNESCO yakihusisha redio za jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani huku washiriki wote wakionyesha kuridhika na mafunzo hayo.
0 comments:
Post a Comment