Mwanasheria kuu wa chama upinzani Chadema nchini Tanzania
Tundu Lissu, ambaye amekuwa akipokea matibabu Nairobi tangu alipopigwa
risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwezi Septemba, amesema
anaamini kushambuliwa kwake kulihusiana na siasa nchini humo.
Akizungumza
na BBC, mbunge huyo wa Singida Mashariki amelilaumu Bunge la nchi hiyo
akisema halijachukua hatua zozote kumsaidia tangu kulazwa kwake
hospitalini.
Makamu wa Rais wa Tanzania Bi Samia Suluhu alimtembelea hospitalini mapema wiki hii.
Bw Lissu amesema anaendelea kupata nafuu vyema.
Juhudi za BBC za kuwasiliana na msemaji wa Bunge la Tanzania kuhusu tuhuma za Bw Lissu hazijafua dafu.
Amezungumza na mwandishi wa BBC John Nene.
0 comments:
Post a Comment