Ikiwa tar 10 ni siku ya kilele cha maadili
duniani elimu imetolewa juu ya
kutoa na kupokea Rushwa na Taasisi ya
kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru
kwa wakuu wa Idara wilayani makete mkoani njombe na .
Elimu hiyo imetolewa
mapema hii leo katika ukumbi wa halmashauri bwana Emmily Okelo wa ofisi
ya kupambana na rushwa [Takukuru] wilayani makete kwa niaba ya mkuu wa takukuru
wilaya amesema katika kilele cha kuazimisha siku ya maadili ambayo inaazimishwa kaunzia tar 6 disember hadi tar 10 ya mwezi
desemba ambapo ndo kilele cha maadhimisho hayo
Bwana OKELO amewataka wakuu wa idara mbalimbali katika
halmashauri ya wilaya ya makete kuwa na wajibu wa kulinda Rasilimali fedha na
vifaa huku kauli mbiu yake kwa mwaka
huu ikiwa inasema wajibika pinga vitaRushwa,zingatia
maadili,haki za binadamu kuelekea uchumi wakati.
Pia amesema
wananchi na wafanyakazi wanatakiwa kufuata maadili na utii wa sheria ya
kuzuia na kupambana na rushwa
TAKUKURU sheria namba 11 ya mwaka
2017 na wananchi wanatakiwa kuisoma ili kuielewa vizuri.
Ofisi ya takukuru
Imesema wananchi na
wafanyakazi wanahaki na wajibu wa kutembelea ofisi ya kupambana na rushwa Takukuru kujifunza baadhi ya vitu,
kuomba ushauri,na mapendekezo na watayapokea kwa kuyafanyia kazi.
Naye mkurugezi wa
halmashauri ya wilaya ya makete Ndugu Francis E Namaumbo amewashukuru
ofisi ya kupambana na rushwa takukuru kwa kutoa elimu na amewashauri
wafanyakazi na wananchi kutoa ushirikiano kwa ofisi hiyo kwa kuwapa mialiko mbalim bali ili kuweka
ukaribu nao.

0 comments:
Post a Comment