Zoezi
la kupokea miili hiyo limeongozwa na Waziri wa Ulinzi Dkt. HUssein
Mwinyi, na maaskari wengine wa JWTZ ambao walishusha miili hiyo na
kupiga gwaride mbele ya miili ya askari hao.
Baada
ya miili hiyo kupokelewa uwanja wa ndege itapelekwa katika hospitali ya
jeshi ya Lugalo ili kuwapa fursa maafisa kuifanyia uchunguzi miili
hiyo, kabla ya kutangazwa kwa tarehe ya mazishi.
Ijumaa
ya Desemba 8 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa
taarifa ya vifo vya askariu hao ambao walikuwa nchini Kongo kulinda
amani, huku 44 wakijeruhiwa vibaya, 8 wakiwa mahututi na wawili
hawajulikani waliko.

0 comments:
Post a Comment