
Mahakama ya mwanzo Makete
imemhukum Bi, HURUMA KYANDO (26) mkinga mkulima,mkristo mkazi wa kijiiji cha Bulongwa
wilaya ya Makete mkoani Njombe kulipa faini ya shilingi milioni moja (1000,000/=)au
kutumikia kifungo gerezani miezi sita na fidia ya shilingi laki mbili kwa
kosa la kumfanyia ukatili mtoto wa miaka
11 aneyesoma darasa la tano shule ya msingi Bulongwa.
Mshitakiwa alitenda kosa
hilo la kumfanyia ukatili mtoto kinyume na kifungu cha 21 na 14 cha sheria ya
mtoto namba 21 ya mwaka 2009.
Kosa hilo lilitendeka mnamo
tarehe 25/11/2017 huko katika kijiji cha Bulongwa ambapo mshitakiwa
alimtumbukiza mtoto huyo kwenye shimo la choo kwa kumfunga kamba ya manira
tumboni kwa lengo la kumtoa mbuzi aliyekuwa ametumbukia katika shimo hilo hivyo
kumsababishia maumivu makali na kuhatarisha uhai wake.
Baada ya kusomewa shitaka
hilo mtuhumiwa alikili kutenda kosa hilo hivyo mahakama kumtia hatihani na
kutoa hukum hiyo.
0 comments:
Post a Comment