Diamond
Platinumz ,Akiwa kama Msanii mkubwa nchini ameomba radhi mashabiki
wake ambao walikuwa wamekaa wakimsubiri kwa hamu katika shoo
iliyoandaliwa na Mh. Paul Makonda huku ikihusisha wanafunzi wa mwaka wa
kwanza kutoa vyuo vyote Dar Es Salaam , show hiyo ambayo ilikuwa
ikifanywa na kushiriki kwa wasanii wengi wakubwa na wakongwe ilitegemewa
kuwa Diamond atakuwa ni mmoja ya wasanii watao kwenda ku-perfom katika
jukwaa hilo lakini haikuwezekana.
Siku
iliyofuata Diamond Platinumz alitumia ukurasa wake wa instagram
kuwaomba radhi mashabiki wake wote ambao hata yeye mwenyewe alitumia
njia kubwa kuwahasisha waweze kutokea alafu yeye akashindwa kutokea.
Najua wengi mlikuwa ma shaulu ya kuona uwepo wangu pale mlimani city jana.. ila amini kabisa kuwa hata mimi nilikuwa nina shauku zaidi ya ile ya kwenu, ya kuimba na kufurahi pamoja nanyi, na shauku iyo ilikuwa kubwa kuliko yenu na ndio maana nilitumia jitihada sana kuwahamasisha ili muwepo kwa wingi katika tamasha hilo ili tufike kwa wingi pale , lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu nilishindwa kufika pale,hivyo tusisononeke wala kuchukukia , naomba radhi na kuwapa pole wale wote waliokwazika jana ,Inshallah Mwenyezi Mungu siku akiniandikia kuwa na nyie ntawaarifu-Alifunguka Diamond
Show
iyo ilikwenda vizuri na kufana sana kutokana na uwepo wa wasanii wengi
wakubwa na wakongwe akiwepo AY,Mwana FA, Fid Q, Lady jay dee, rich
mavoko.Lakini katika tamasha hilo wasanii lady jay dee na mwana Fa
walionekana kwa mara ya kwanza wakiwa wote jukwaani tangu
walipokorofishana miaka mingi iliyopita na kupata mwaka huu
0 comments:
Post a Comment