Mtoto
wa miaka saba aliyelelewa kama mtoto wa kike kutokana na maumbile yake
kutoeleweka vema, baada ya vipimo vyote katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), ameonekana kuwa ni mwanamume, hivyo amefanyiwa upasuaji
wa kwanza wa kushusha kokwa (mbegu za kiume) kwenda kwenye korodani ili
kumrejesha katika hali ya kawaida.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Watoto MNH, Zaitun Bokhary alisema hayo
alipofanya mahojiano maalumu na HabariLeo kuhusu kambi ya wiki moja
iliyowekwa kwa ajili ya kufanya upasuaji ambao ni mgumu, wakishirikiana
na wataalamu watano kutoka Chuo Kikuu cha Oxford nchini Marekani.
Dk
Bokhary alisema upasuaji huo ni hatua ya kwanza katika kumrejesha mtoto
huyo katika hali ya kawaida, hatua nyingine za upasuaji zitafuata,
kwani atafanyiwa upasuaji kwa hatua tatu.
Alisema
kwa kuwa mtoto huyo vipimo vimeshaonesha kuwa ni wa kiume, wametoa
ushauri kwa wazazi wake hususan baba yake kuwa karibu na mtoto huyo ili
kumfanya asijisikie vibaya, kwani awali alikuwa akijisaidia haja ndogo
kama mtoto wa kike, pia alikuwa amepewa jina la kike ikiwa ni pamoja na
kuvaa nguo za kike.
“Tumemshauri
baba yake kutembea mara kwa mara na mtoto wake, pia kwenda naye katika
michezo ya kiume, ikiwa ni pamoja na kuanza kumvalisha mavazi ya kiume.
“Mtoto huyu alipoanza kuvaa nguo za kiume kwa mara ya kwanza alikuwa
akijisikia aibu kwa kuwa alishazoezwa mambo ya kike, lakini tunaendelea
kutoa ushauri kwa wazazi ili wawe karibu na mtoto wao asijisikie tofauti
yoyote,” alisema daktari huyo.
Aliongeza kuwa tayari mtoto huyo alikuwa akisoma katika shule ya msingi
mojawapo jijini Dar es Salaam, hospitali hiyo inafanya utaratibu kupitia
kwa daktari wake ili kuandika barua kwa Wakala wa Usajili Ufilisi na
Udhamini (Rita), atambuliwe kama mwanamume, ikiwa ni pamoja na
kuhamishwa shule aliyokuwa akisoma.
Alisema
kuwa na sasa mtoto huyo, amehamishwa nyumbani kwao anakaa na ndugu zake
eneo lingine ili aanze kuzoea mazingira mapya ya maumbile yake. Pia Dk
Zaitun alielezea upasuaji mwingine mgumu uliofanyika ni wa mtoto wa siku
mbili ambaye alikuwa na tatizo katika mfumo wa nyongo, njia ilikuwa
imefungwa ilibidi apasuliwe kufungua njia ili mfumo wa nyongo uendelee
kama kawaida.
“Kwenye
mfuko wa nyongo kulikuwa kumetengeneza uvimbe nyongo isipite vizuri,
hivi sasa baada ya upasuaji anaendelea vizuri,” alisema. Daktari bingwa
huyo wa upasuaji wa watoto, alieleza upasuaji mwingine walioufanya ni
kwa mtoto aliyekuwa na saratani ya figo zote mbili, moja ilitolewa na
nyingine ilikuwa haijalika ikaondolewa sehemu ya tatizo bila kuathiri
mfumo wa misuli.
Alisema
upasuaji wote huo umekwenda vizuri, hali za watoto hao zinaendelea
vema. Alisema kambi ya upasuaji hiyo ilikuwa Novemba 27 hadi Desemba
Mosi, mwaka huu iliongozwa na Daktari Bingwa Mshauri Mwelekezi wa
Upasuaji wa Watoto, Profesa Kokila Lakhoo kutoka Chuo Kikuu hicho cha
Oxford. Alisema Dk Lakhoo amekuwa akija hospitalini hapo kila mwaka,
kusaidia ule upasuaji ambao ni mgumu, na huu ni mwaka wake wa tano
kufika nchini.
0 comments:
Post a Comment