Polisi
nchini India wanasema wamemkamata mwanamume mmoja ambaye uvundo wa
soksi zake ulisababisha ugomvi kati yake na abiria wenzake kwenye basi.
Waliambia BBC kwamba wamewasilisha kesi dhidi ya Prakash Kumar, 27, kwa “kuvuruga amani ya umma”.
Kisa hicho kilitokea kwenye basi lililokuwa safarini kuelekea mji mkuu Delhi, baada ya Kumar kuvua viatu vyake na soksi.
Harufu
mbaya kutoka kwenye soksi zake ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba abiria
walimuomba Bw Kumaru kuziweka ndani ya mkoba wake au kuzirusha nje ya
basi.
Lakini anadaiwa kukataa hilo, na ugomvi mkali ukazuka.
Abiria
kisha walimlazimisha dereva wa basi hilo kuingia kituo cha polisi
katika jimbo la Himachal Pradesh, kaskazini mwa India, ambapo
malalamishi dhidi yake yaliwasilishwa.
Gazeti
la Hindustan Times limemnukuu Bw Kumar akisema kwamba soksi zake
hazikuwa na harufu mbaya, na kwamba abiria wenzake waligombana naye “bila sababu”.
Polisi wameambia BBC kwamba mwanamume huyo amepewa dhamana.
0 comments:
Post a Comment