Hatimaye
Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa rasmi kwa muhula wa pili wa miaka mitano
katika sherehe zilizofana kwenye Uwanja wa Kasarani mwezi mmoja baada
ya kuibuka mshindi wa uchaguzi uliosusiwa na mpinzani mkuu Raila Odinga.
Kulikuwa
na nderemo na shangwe katika uwanja huo kutoka kwa maelfu ya wananchi
wengi wao wafuasi wa muungano wa chama tawala cha Jubilee waliojaa
kwenye Uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Moi, Kasarani.
Uwanja
huo unaingiza watu 60,000 lakini habari zinasema walioingia walikuwa
100,000. Wageni waalikwa na watu mashuhuri wapatao 40 walihudhuria
sherehe hizo wakiwemo zaidi ya viongozi wakuu wa nchi 10.
Kenyatta,
55, alishinda uchaguzi mkuu wa marudio wa Oktoba 26 kwa asilimia 98.
Uchaguzi huo ulifanyika baada ya matokeo ya ushindi wa Agosti 8 kufutwa
na Mahakama ya Juu kwa maombi ya Odinga aliyewasilisha ushahidi wa
dosari na ukiukwaji wa katiba.
0 comments:
Post a Comment