
Rais wa Tanzania
John Pombe Magufuli amemtuma makamu wake wa rais kumwakilisha katika
sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta nchini Kenya.
Rais
Magufuli ambaye awali alikuwa amethibitisha kuhudhuria sherehe hiyo na
hata kutuma taarifa kwa vyombo vya habari sasa amemtuma makamu wake Mama
Samia Suluhu Hassan kumwakilisha.
Uhusiano kati ya Kenya na
Tanzania umeonekana kudorora siku za karibuni hasa kufuatia kupigwa
mnada kwa ng'ombe zaidi ya elfu moja kutoka Kenya waliokuwa wameingizwa
Tanzania. Tanzania kadhalika ilichoma moto vifaranga waliodaiwa kutoka
Kenya.
Tayari
kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Edward Lowassa ambaye ni rafiki
mkubwa wa rais Uhuru Kenyatta amewasili katika uwanja wa Kasarani tayari
kwa sherehe hiyo.
Rais Magufuli ni mwandani wa karibu wa kiongozi
wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ambaye alisusia uchaguzi wa
marudio wa Oktoba 26 ambao Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi kwa kujipatia
asilimia 98 ya kura zilizopigwa.
Tayari makamu huyo anatarajiwa kuwasili katika uwanja wa Kasarani wakati wowote sasa
0 comments:
Post a Comment