Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo
Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea ma kumjulia hali Mbunge wa Singida
Mashariki kupitia CHADEMA, Tundu Lissu anayepatiwa matibabu jijini
Nairobi Kenya.
Makamu
wa Rais ambaye alikwenda Kenya mapema leo asubuhi kwa ajili ya
kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa aliyekuwa Rais Mteule wa Kenya,
Uhuru Kenyatta, alifika hospitalinia hapo mapema leo jioni majira ya saa
11.
Samia
Suluhu alifika kumjulia hali Tundu Lissu akiwa ameambatana na Balozi wa
Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana pamoja na maofisa wengine.
Makamu wa Rais alikuwa njiani kurejea nchini Tanzania wakati alipofika hospitalini hapo.
Tundu
Lissu amelazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu Septemba 7 baada ya
kujeruhiwa kwa kushambuliwa kwa risasi akiwa mjini Dodoma eneo la Area
D.
Kwa
mujibu wa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Lissu alishambuliwa kwa zaidi ya
risasi 30 ambapo risasi 5 tu ndizo zilimpata katika maeneo ya mkononi,
tumboni na mguuni.
Makamu
wa Rais amekuwa kiongozi mwandamizi wa serikali wa kwanza kumtembelea
Lissu hospitalini hapo. Wengi ambao wamekuwa wakimtembelea ni wabunge
wenzake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
0 comments:
Post a Comment