Home » » Shule zilizofanya Vizuri Makete zapewa Tuzo leo

Shule zilizofanya Vizuri Makete zapewa Tuzo leo

Unknown | Friday, November 17, 2017 | 0 comments
Shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha 6 mwaka huu katika wilaya ya Makete mkoani Njombe zimepewa tuzo na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri na kukabidhiwa mbele ya baraza la madiwani hii leo

Akikabidhi tuzo hizo Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Veronica Kessy amezipongeza shule hizo kwa jitihada walizozifanya kuhakikisha wanafunzi hao wanafanya vizuri na kuiletea sifa wilaya ya Makete

Awali Afisa elimu Sekondari wilaya ya Makete Jacob Meena ametolea ufafanuzi wa namna shule hizo zilivyofanya vizuri kiwilaya, kimkoa na kitaifa hadi kupelekea uongozi wa halmashauri kutoa tuzo hizo kwa shule husika


Baadhi ya wakuu wa shule waliozungumza na Eddy Blog akiwemo Ekson Ntulo wa Bulongwa sekondari, Mkuu wa shule ya Mwakavuta na Iwawa baada ya kupokea tuzo hizo wameelezea namna walivyojisikia kupokea tuzo hizo na wakiahidi kufanya vizuri katika mitihani mingine inayokuja lengo likiwa ni kuinua kiwango cha elimu katika shule zao na taifa kwa ujumla


Shule za sekondari zilizokabidhiwa tuzo hizo ni Lupalilo, Iwawa, Mwakavuta, Itamba na Bulongwa
 Mkuu wa shule ya sekondari Bulongwa akionesha tuzo yao

 Mkuu wa shule ya sekondari Lupalilo akipokea Tuzo
 Mwakilishi wa mkuu wa shule Iwawa sekondari akionesha tuzo yao
 Mkuu wa shule ya sekondari Mwakavuta akiwa na walimu washule hiyo wakionesha tuzo yao
 Mwakilishi wa Mkuu wa shule ya Iwawa sekondari akifanya mahojiano mbashara na vyombo vya habari baada ya kupokea tuzo
Mkuu wa shule ya sekondari Mwakavuta akifanya mahojiano mbashara na vyombo vya habari baada ya kupokea tuzo
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy (wa pili kulia) akiwa ameshika moja ya tuzo kabla ya kumkabidhi mhusika
Mkuu wa shule ya sekondari Bulongwa akifanya mahojiano mbashara na vyombo vya habari baada ya kupokea tuzo
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG