Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy akizungumza kwenye baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Makete hii leo
Serikali imetoa msisitizo wa mambo kadhaa yanayotakiwa kutekelezwa wilayani Makete mkoani Njombe kama sehemu ya Tanzania ili kurahisisha gurudumu la maendeleo kama inavyotakiwa
Akizungumza katika baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete hii leo Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Veronica Kessy ameyataja baadhi ya mambo na kuyatolea msisisitizo na kuwaomba waheshimiwa madiwani kuyasimamia katika maeneo yao
Mkuu huyo wa wilaya ameagiza umuhimu wa kila kijiji kuwa na zahanati na kata kuwa na kituo cha afya huku akiagiza wataalamu kuainisha vijiji ambavyo kwa mujibu wa sera ya afya havitakuwa na zahanati kutokana na kuwepo kituo cha afya au hospitali katika vijiji hivyo
Ameshangazwa na kata zote 23 za wilaya ya Makete, kata 5 pekee ndizo zenye vituo vya afya wakati sera inataka kila kata iwe na kituo cha afya hivyo jitihada ziongezeke kujenga vituo hivyo
Kuhusu uharibifu wa mazingira uliotokana na utorokaji wa moto kichaa na kusababisha madhara ikiwemo kifo cha mwananchi, mkuu huyo ameliagiza baraza la madiwani kutunga sheria mpya kuhusu moto ambayo itarekebisha mapungufu yaliyopo kutokana na yale yanayoendelea kujitokeza
Pamoja na hayo Mh Mkuu wa wilaya amezungumzia suala la uanzishwaji wa viwanda Makete, ujenzi wa miundombinu kwa shule zote za msingi na sekondari, watu kushiriki kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao kwa kuwa yapo maeneo muamko ni mdogo, tahadhari ya ugonjwa wa kipindupindu, hatua kuchukuliwa kwa mifungo ya nje ya nchi kuingia Makete pamoja na wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye vitambulisho vya taifa
Wakizungumza baada ya Maagizo hayo Diwani wa Kipagalo Mh. Reuben Mwandilava pamoja na Diwani wa Ipelele Mh Mwipelele Mbogela wameahidi kuyatekeleza maagizo yote ya Mkuu wa wilaya
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa akatolea msisitizo unaoendana na kumshukuru Mkuu wa wilaya kwa maagizo yake hasa suala la sheria ya utoroshaji wa moto
0 comments:
Post a Comment