Wafanyakazi mkoani njombe wameiomba serikali
kuwaongezea watumishi wa umma mishahara
na kulipa malimbikizo ya mishahara kwa wafanya kazi pamoja na kupandishwa madaraja
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi hii leo
katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo katika mkoa wa njombe
yamefanyika wilaya ya makete viwanja vya mabehewani Makete mjini katibu wa
shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania [TUCTA] ambaye pia ni
katibu wa chama cha walimu mkoa wa
njombe [CWT] FRANTEN KWAHHISON amesema hali ya maisha ya mtanzania imekuwa ikipanda kila siku lakini mishahara
ya watumishi imekuwa haiendani na maisha halisi.
Sambamba na hilo wameiomba serikali kupandisha
mishahara ya watumishi waliopandishwa vyeo kuanzia mwaka 2016 kwani watumishi
hao ni haki yao ya kupandishwa mishahara ili waongeze ufanisi Mzuri wa ufanyaji
kazi.
Vyama shirikisho vya wafanyakazi mkoa wa njombe vimeishukuru
serikali ya awamu ya tano kwa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard geurge, kuwarudisha watendaji wa
vijiji ambao walikosa sifa kutokana na kutokuwa na vyeti vya kidato cha nne huku
wakiipongeza serikali kwa usimamizi mzuri wa uchumi wa nchi.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi katika mkoa wa njombe alikuwa ni
mkuu wa mkoa wa njombe mh CHRISTOPHA OLE SENDEKA katika sherehe hizi
amewakirishwa na mkuu wa wilaya ya makete mh VERONIKA KESSY kwa niaba ya mkuu
wa mkoa amesma changamoto zote ambazo
watumishi wanakumbana nazo serikali ya awamu ya tano itazishughulikia ikiwemo
malimbikizo mbalimbali ya mishara ya watumishi pamoja na fedha ya uhamisho kwa
watumishi huku akiwaomba wafanyakazi kuwa wavumilivu maana serikali ya dakta
john pombe magufuli ni sikivu itatatua changamoto hizo.
Veronika kessy amewaomba wananchi wa mkoa wa
njombe pamoja na wafanya kazi kwa ujumla kutambua kuhusu ugonjwa wa virusi vya ukimwi [VVU] ambao umekuwa ni janga kubwa
katika mkoa wa njombe na amewaomba kwenda vituo vya afya kujitokeza kupima
ugonjwa huo.
Maadhimisho hayo yameambatana na kaulimbiu
isemayo KUUNGANISHWA KWA MIFUKO YA
HIFADHI YA JAMII KULENGO KUBORESHA MAFAO YA WAFANYA KAZI.
baadhi ya picha za mei mosi
0 comments:
Post a Comment