Wakili wa kujitegemea ROSEMARY WAMBALI ametoa elimu juu ya maswala ya haki za Binadam kwa jamii kupitia kipindi cha sheria kinachorushwa na kitulo fm Redio Makete mkoani Njombe kila siku ya jumatatu saa moja na dakika kumi na tano,
Akizungumza na wananchi juu ya haki za Binadam amefafanua kuwa kila Binadam ana haki zote za msingi,huku akizitaja baadhi ya haki hizo hizo kuwa ni pamoja na haki ya kuishi,haki ya kuabudu,haki ya kwenda popote kwa kuzingatia taratibu,haki ya kupata elimu,haki ya kutoa maoni na mawazo,haki ya kupata na kutoa habari,
Wakili Wambali ameongeza kusema kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa haki za Binadamu hasa kwa watoto ambapo amesema jamii wametumia mitandao ya kijamii vibaya kuweka "kupost" picha za watoto waliofanyiwa ukatili kama vile kubakwa pamoja na picha za ajali zikionyesha majeraha ya majeluhi jambo ambalo amesema niukiukwaji wa haki za binadam.
0 comments:
Post a Comment