Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe
ameupongeza uongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuongeza
usikivu katika maeneo mbalimbali ya mipakani mwa nchi.
Mheshimiwa
Mwakyembe ametoa pongezi hizo alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la
wafanyakazi wa Shirika hilo uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam
ambapo katika mkutano huo walijadili mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya
bajeti na mwenendo wa shirika hilo.
“Ninafuraha
kubwa kupata taarifa ya kuimarika kwa usikivu katika maeneo ya mipakani
yaliyokuwa na yanasumbua kwa muda mrefu kama maeneo ya
Tarakea,Kibondo,Longido,Tarime na Mbababey na pamoja na maeneo ya Mtwara
na Nachingwea,”Dkt.Mwakyembe.
Akiendelea
kuzungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Waziri Mwakyembe aliendelea
kupongeza uongozi wa TBC kwa kufanya maamuzi ya kutumia mafundi mitambo
wa ofisi yao kwa ajili ya kufunga mitambo hiyo pamoja na kufanya
matengenezo pia aliwapongeza mafundi mitambo waliofanya kazi hiyo kwa
uaminifu na uzalendo huku akiomba uongozi wa shirika hilo kuwapeleka
bungeni mafundi hao wakati wa bunge la bajeti.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba
alieleza kuwa mpaka sasa Wilaya ya Geita tayari kumeshafungwa mitambo
mipya inayosaidia kuboresha usikivu kwa uhakika na kazi hiyo imefanywa
na mafundi wazalendo wa shirika hilo.
Naye
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC Bw. Joseph Kambanga
alieleza kuwa mpaka sasa kazi ya kububoresha usikivu inaendelea na
baadhi ya mafundi walikuwa Tarime wakiendelea na kazi hiyo na kwa mwezi
ujao wanategemea kuongeza usikivu kwa Mkoa wa Mtwara na Nachingwea .
Pamoja
na hayo Waziri Mwakyembe ameuagiza uongozi wa TBC pia kufichua uovu
uliyoko katika jamii kwani serikali ya awamu ya tano inapiga vita
ufisadi na matendo maovu katika jamii hivyo wasibaki nyuma katika
kuyaangazia hayo pale wanapohabarisha umma.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe
akiwapongeza viongozi na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania kwa
kuongeza usikivu kwa maeneo ya mipakani (hawapo
pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi
uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba.
Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt.Ayoub Rioba akitoa taarifa ya upanuzi wa usikivu wa matangazo ya Shirika hilo nchini kwa Mheshimiwa
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe
(Kushoto) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi
uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment