Mbunge wa jimbo la Makete Prof. Norman Adamson Sigara King amechangia mifuko ya saruji zaidi
ya sabini (70) kwa ajili ya kumalizia jengo la maabara pamoja na
mabati mia moja kwaajili ya kuchangia ujenzi wa madarasa ya Shule ya
Secondari ya Isapulano Ambayo kwa sasa imeshaanza Rasmi.
Mh.Sigara
ametoa Mchango huo alipo kuwa akiwasilisha hati ya usajili wa shule
hiyo kwa wananchi ambao kwa kipindi cha miaka mingi walikuwa wakipata
huduma ya shule kwa umbali mrefu hivyo kupelekea gharama za maisha kuwa
juu kila siku.
wananchi
wa kata ya Isapulano wamesema kuanza kwa shule hiyo kumefuta machozi ya
mudamrefu ambapo kwasasa wamehamasika kupeleka watoto wao shule huku
wakimshukuru mgunge kwa kushirikiana na halmashauri kufanikisha
kufunguliwa kwa shule hiyo
Tazama video hiyo
Mh: Mbunge Prof Sigara akizungumza na wananchi wa Isapulano
Mbunge akiahidi mchango wake huku akisisitiza kauli mbiu yake ya kazi kwanza maneno baadaye
0 comments:
Post a Comment