SHIRIKA
la umoja wa Kimataifa la Elimu,Sayansi,Mazingira na Utamaduni-UNESCO-Limewataka
waandishi wa habari za redio za kijamii nchini kutumia mafunzo ya uandishi wa
habari wanayopata ili kufikisha taarifa sahihi na zenye tija kwa jamii inayowazunguka.
Wito
huo umetolewa leo mjini Dodoma na Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la
UNESCO Dar es salaam Bi Faith Shayo
wakati akiongea na waandishi wa habari zaidi ya 40 wa redio za kijamii nchini
wanaomaliza mafunzo yao leo yanayotolewa na shirika hilo katika ukumbi wa
wakala wa ujenzi-TBA-.
Bi
Shayo amesema redio za kijamii zina nguvu kubwa ya kufikisha ujumbe kwa haraka
katika jamii hivyo waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kufanya kazi kwa
weledi ili kuzisaidia jamii zilizoko pembezoni ili ziweze kufikia malengo ya
maendeleo ya millennia.
Sambamba
na hayo amewataka waandishi wa habari kuandika habari zenye uzania ili kuondoa
migogoro katika jamii ikiwa ni pamoja na kuyafikia makundi maalumu ambayo mara
nyingi yamekuwa yakitengwa .
Kwa
upande wake Afisa wa mawasiliano wa Tume ya Taifa ya UNESCO(NATCOM) Bi Cristina ametoa wito kwa waandishi wa habari
kutumia vizuri mafunzo ya Tehama ili kuwarahisishia kusambaza habari kwa
urahisi katika jamii kulingana na kasi ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
Semina
hiyo ya siku 12 iliyojumuisha waandishi wa habari 49 wa redio za kijamii 24
nchini,imelenga kujifunza namna ya kuandika habari za uchunguzi,kutangaza
habari za michezo kwa kuzingatia jinsia ikiwa ni pamoja na kujifunza namna ya
ufuatiliaji na tathimini ya taarifa za habari.
0 comments:
Post a Comment