Mwalimu
Mkuu shule ya Msingi Ihanga iliyopo kijiji cha Ihanga kata ya Ukwama
Wilayani Makete Mkoani Njombe Mwl.Amos Mpandila kwa kushirikiana na
Kamati ya shule hiyo chini ya Mwenyekiti wake Fedick Sanga wanatuhumiwa
kutumia vibaya fedha za ujenzi wa choo cha wanafunzi kwa kubadilisha
matumizi na kusababisha ujenzi huo kusimama na kuleta sintofahamu kubwa
kwa Wananchi
Fedha hizo zaidi ya Milioni 4 zimetumika
isivyo baada ya kutakiwa kujenga choo chenye mashimo manne badala yake
ukafanyika ukarabati uliochini ya kiwango tofauti na Maelezo yaliyomo
kwenye mwongozo wa ujenzi wa choo (BOQ)
Mwenyekiti wa
kijiji hicho Bw.Fedenicko Ndelwa amesema fedha hizo zilitakiwa kununua
mchanga kutoka Makambako lakini haujanunuliwa badala yake wanafunzi
wakaagizwa kutafuta mchanga porini,tanki la maji lilitakiwa linunuliwe
lenye ujazo wa Lita elfu 5 lakini limenunuliwa lenye ujazo wa Lita elfu
2,bati halijanunuliwa hata moja zimetumika chakavu n.k
Kamati
ya uchunguzi iliyoundwa na Mh.Diwani wa kata ya Ukwama Augustino Tweve
ikabaini mapungufu mengi tu na kumlazimu Diwani huyo kuitisha mkutano na
wananchi wa kijiji hicho uliotawaliwa na wananchi wenye jazba wakitaka
kujua matumizi ya fedha hizo
Mwalimu mkuu alipoulizwa na
kamati hiyo aliieleza kuwa"Samahani nakiri kosa kwa kutumia fedha
zingine kununua miti ya parachichi na mbolea yake tofauti na mwongozo wa
matumizi ya fedha hizo"
"Fedha zingine laki moja na
elfu sitini nilitumia nauli kwenda Makete mjini kuchukua fedha kwa ajili
ya ukarabati wa choo hiki kinyume na mwongozo"
Jambo ambalo wananchi walipingana nalo vikali kwa kukiuka taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali
Kamati
iliyoundwa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mzee Michael Nundu iliendelea
kusema"kamati ya shule imetukimbia kufanya uchunguzi na kushindwa
kuwahoji wakimkimbia hata Mkuu wa shule waliyeshirikiana naye katika
kupanga matumizi hayo kinyume"
Diwani alilazimika
kuiagiza kamati ya shule ndani ya wiki moja ikae na kujadili jambo hilo
ili kurudi kwa fedha za Serikali zilizotumika vibaya lakini Mwenyekiti
wa kamati ya shule bw.Fedick Sanga akagomea kufanya hicho na kusema yupo
tayari kwa lolote lakini hatotekeleza agizo hilo
0 comments:
Post a Comment