KADA
mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ameeleza sababu
zinazochangia kudhoofika kwa vyama vya upinzani nchini.
Amesema
kuyumba kwa vyama hivyo kunachangiwa na ubinafsi waviongozi wake ambao
wengine wamegeuza Chama ni mali yao na kutoa maamuzi ambayo si
shirikishi.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam January 2,Katambi alisema kuwa tangu ameondoka
Chadema ambako alikuwa Mwenyekiti wa Vijana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya
chama hicho amekuwa kimya muda mrefu lakini ameona ni vema akasema mambo
kadhaa kuhusu hali ya kisiasa nchini.
Kuhusu
vyama vya siasa kuyumba, Katambi alisema zipo sababu ambazo zimekuwa
zikichangia vyama hivyo kushindwa kuwa imara na matokeo yake kubaki
kulalamikia kila jambo ambalo linafanywa na Serikali hata liwe lenye
maslahi kwa nchi.
"Upinzani
umeshindwa kujenga chama taasisi kwani hivi sasa kila chama ni cha
mtu.Vyama vingi ni vya watu na si taasisi.Dhana ya taasisi ni kwamba
sheria ,kanuni na taratibu lazima zifuatwe
"Kama
mtu anadharau katiba na misingi iliyowekwa basi huo niudikteta.
Wapinzani kabla ya kukimbilia kugombea udiwani na ubunge wajikite kwanza
kujenga taasisi, kama wameshindwa kuheshimu katiba za vyama vyao
wanapate uhalali wa kudai Katiba,"alisema.
Alisema
sababu nyingine vyama vya upinzani vimekosa uamuzi shirikishi."Chadema
ambayo inajieleza ni chama cha upinzani chenye nguvu kimeshindwa kuwa na
utaratibu wa kuwa na maamuzi shirikishi na hata yanayoamriwa ni maamuzi
ya mtu.Na pia kuna ukiukwaji wa uteuzi wa nafasi ikiwamo za ubunge viti
maalumu ambao umetawaliwana rushwa na kupeana nafasi kirafiki.
"Tatizo
la upinzani hakuna kuheshimiana na ukosefu wa maadili ya viongozi. Kama
Taifa lazima liwe na viongozi wanaozingatia maadili,kwa mfano leo hii
Ukawa wakichukua nchi nani anaweza kuwa WaziriMkuu,"amesema.
Kada
huyo wa CCM, amesema kuwa vyama vya upinzani adui yaomkubwa ni CCM
lakini wameshindwa kuwa na uwazi kwenye mali zaokwani hata Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),akikagua ni lazima atapata hati
zenye shaka kwani fedha za ruzukuzinatumika vibaya.
"Wanaosema
nimenunuliwa wanajidanganya kwani wakati anakwenda chadema wamemnunua
kwa shilingi ngapi. Kuna wabunge zaidi ya 15w ataondoka Chadema na kuna
wajumbe wapo ndani ya chama hicho lakini tayari wameshaondoka ila
wanaingia kwenye vikao ili kutimiza wajibu tu," alisema Katambi.
Alisema
kwa sasa vyama vya upinzani wamekosa ajenda na waliopo huko wanakwenda
tu bora liende na wengine wanajua wakitoka hawataajirika.
"Kukosea
ajenda chadema walikuwa wanasema wanapambana na ufisadi na hata Dr.
slaa aligeukwa kwa sababu ya masilahi ya watu binafsi.Chadema ya Dk.
Slaa kila mtu anaifahamu ilifika wakati akapelekwa Marekani kwa ajili
ya kuandaliwa ili aje kuwa Rais lakini baadaye wakaanza kumtuhumu kwa
usaliti," alisema
Kutokana
na hali hiyo amesema kuwa sasa umefika mwisho wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kwani malengo ya Chadema yametimia kwa kuua nguvu ya
kila chama ili wabaki wao katika upinzani.
0 comments:
Post a Comment