Chadema
kimepata pigo baada ya mgombea wake wa udiwani Kata ya Manzase wilayani
Chamwino Mkoa wa Dodoma, Mashaka Chalo kujiunga na CCM pamoja na
wanachama wengine 131.
Chalo
amehama Chadema siku ya tatu tangu chama hicho kikuu cha upinzani
nchini kuzindua kampeni katika Kata hiyo na kunadiwa jukwaani na mbunge
wa viti maalum, Kunti Majala.
Uchaguzi
wa ubunge jimbo la Siha, Kinondoni na katika Kata 10 nchini utafanyika
Februari 17, 2018. Uchaguzi katika Kata hiyo unafanyika baada ya
aliyekuwa diwani, Peter Madanya (CCM), kufariki dunia mwishoni mwa mwaka
jana.
Mgombea
huyo amehamia CCM Februari 4, 2018 katika kijiji cha Manzase wakati wa
uzinduzi wa kampeni za chama hicho na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (Bara), Rodrick Mpogolo.
Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde amesema uamuzi wa Chalo kujiuzulu ni ushindi kwa chama tawala.
“Mpogolo
unaweza kufungua kampeni hizi na kisha kuzifunga maana kazi imekwisha.
Tulikuwa na wagombea watatu, lakini kuondoka kwa huyu, CCM tunaona
kazi imekwisha. Wagombea wengine waliobaki hata tukilala usingizi
hakuna kitu ushindi ni wetu,” amesema.
Mgombea wa CCM katika Kata hiyo ni Amosi Mloha.
Lusinde amesema Chadema walimpitisha Chalo dakika za mwisho kuwania udiwani bila kujua kuwa alikuwa pandikizi la CCM.
Akizungumza katika mkutano huo Chalo amesema amerejea CCM kwa sababu ni chama chake na kimemlea.
0 comments:
Post a Comment