Msanii
wa filamu Wastara Juma amepaza sauti yake ya kutaka kusaidiwa pesa ya
matibabu na Rais John Pombe Magufuli baada ya kutapeliwa na kampuni moja
ya simu ambayo ilimteua kama balozi wa bidhaa zao.
Muigizaji
huyo amedai ametapeliwa zaidi ya tsh milioni 80 na kampuni hiyo ya simu
pesa ambayo amedai alikuwa anajichanga kwaajili ya matibabu ya mguu
wake nchini India.
Taarifa ya Wastara.
“RAIS MHE MAGUFULI
MAKAMO MHE SAMIA SULUHU
WAZIRI MKUU MHE KASIM MAJAALIWA
MKUU WA MKOA MHE POUL MAKONDA
WATANZANIA WENZANGU
Mim
Wastara juma muigizaji wa filamu tanzania naandika ujumbe huu mfupi
sina budi sina jinsi nahitajika kurudi hosptal india Sifael hosptal
tokea tal 12/02/2017 ambapo nilitakiwa nifanye matibabu kwa mda wa miaka
2 chini ya uwangilizi wa hosptal hiyo kabla ya kufanya maamuzi ya
kufanyiwa operetion ya mgongo hivyo kila tal 12/ 2 natakiwa kurudi
hosptal nimejitahidi kupambana peke yangu kutafuta pesa ya kunirudisha
hosptal nimeshindwa
Mwezi
1 wachina wenye kampun ya simu ya KZG wamenikimbia nikiwadai milion 80
mwezi wa 2 muzambiq nimepoteza mzigo wa milon 19 kwenye vurugu la
kufukuzwa watanzania
Mwezi
wa 3 nimeenda nchini sweden kufanya filamu nimerudi mikono mitupu mwezi
wa 4 nimedai pesa yangu steps tumeishia kwenda mahakamani bila kulipwa
nilivyokuwa natarajia tokea hapo chchote ninachofanya kinachohusu pesa
lazima tuishie polisi au mahakamani silipwi vile tunavyokubaliana na
baya zaidi ninaofanya nao kazi awajui kuwa tokea nimerudi nchini toka
sweden ninahaha kutafuta pesa ya matibabu,,
silali
kwa maumivu makali ya mgongo na ninazimia kila mda hii imetokana na
kuchelewa kurudi hosptal kufanya tiba ya mgongo na kubadilisha soberly
skoner inayowekwa kwenye mguu kama tiba kuu ya kurudisha mgongo wangu
ukae sawa matokeo yake mguu unavimba na kuchanika kila mara mgongo
unauma kitu ambacho kinanikosesha raha kabisa na kuona sasa naathirika
kiakili kwa maumivu sababu mda mwingi nakunywa dawa za maumivu bila
kujua kama nimemeza dawa mara ngapi kwa siku hii sio nzuri kiafya
Kikubwa
ninachoomba kutoka kwenu ni mim nirudi kwenye apointment yangu ya
hospital sababu siwezi kurudisha mguu wangu kama zamani lakini ninaweza
kuyakwepa maumivu kutokana na tiba ninayoweza kupata kupitia tatizo
langu
Sihitaji
msaada wa mtu nikiwa mahututi nikiwa siwezi kuandika sms kupokea sim au
kumtambua mtu nahitaji sasa ninayo nguvu kidogo ya kuelewa hta nataka
kutibiwa nin staki nisaidiwe kwa mtu kunisemea matatizo yangu wakati huo
mim nimeshashindwa hta kuongea tena please watanzania wenzangu mficha
uchi hazai sio mim mwenye matatizo pekee wapo wengi ila wanaona aibu
najua mtajiuliza kiasiku wastara anauza nguo why?
anataka
msaada sio kweli kuwa biashara ya mtandao inakidhi mahitaji yetu
nimekuwa nikipost bidhaa kwa fujo bila kupost hta picha zangu nikiamini
nitauza sana ili nirudi hosptal lakini sio kweli kabisa watu wanataka
kuniona mim mitandaoni na sio mashati na magauni ninayouza ndio maana
sifanyi vizuri upande huo ninaumia sana kuona mashabiki nawanyima haki
ya kuniona lakini ninayo shida nahitaji niwe na afya njema nitembee
vizuri nifurahi na watoto wangu na mashabiki zangu
afya
yangu mim inauzwa tena kuanzia dollar 18000 pia mtajuliza why sioni
aibu kusema shida zangu au kuomba msaada wakati mimi ni msanii na tafsir
ya walio wengi wasanii ni watu wenye pesa sana sio kweli sanaaa yetu
ndio kwanza inakuwa nimechoka kupost nikilalamika naumwa huku kesho mtu
ananiona mzima nacheza mziki kumbe najilazimisha tu kuficha mateso yangu
staki tena kuficha maumivu yangu natembea nanenepa huku nina maumivu
makali
natamani nimmpe mtu huu mwili na ili jina ili niwe huru kwenye mateso ya kujificha huku naumia
nimejaribu
sana kuongea na marafiki zangu wa karibu wanajua natania ninavyosema
naumwa nahitaji msaada mtu aamini hata nikimwambia nichangie elfu 50
anaona nina pesa nyingi sana nadanganya No kabla haujafa haujaumbuka
nikiuza
nyumba gari na chchote nilichonacho alafu nikafa watoto wangu wataishi
wapi nin kitawasaidia mpka wapate pesa za kujikimu?? Jibu hakuna japo
nimejaribu kunadi kilakitu nilichonacho ili mladi nipate pesa nirudi
hosptal lakin mda umepita sana na naendelea kuumia mwili na kiakili pia
sijafanikiwa please usinitafsir vibaya wala kunikejili wakati huna uwezo
wa kunisaidia mim nimeamua kuwa muwazi kuwa nahitaji msaada ili
niendelee na majukumu yangu watoto na watanzania waendelee kuniona
Pili
ninaomba serikali inisaidie nipate pesa ninazowadai wachina mpka sasa
zaidi ya milion 400 maana nilisain mkataba wa miaka miwili mpka leo ni
mwaka 1 na miezi 2 na awajasitisha huo mkataba mpka leo kitu
kinachoniuzia mim kufanya kazi na kampuny nyingine ya kuuza sim mpka
mkataba wao uishe na awajanipa hta shilingi mia mpka sasa….
please
wamenitoroka sina mkono mrefu wa kuwakamata zaidi ya huruma yenu na
wanacho kiwanda kikubwa tu uko kwao china cha KZG kwasasa ninachohitaji
kuliko chochote ni afya yangu kwanza
Ukiguswa kwa chchote nipo na unanipata kwa no hii.
0768666113
0768666113
0 comments:
Post a Comment