Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa njombe
mh Jasery mwamwala amewaomba wazazi na walezi mkoa wa njombe kutoa ushirikiano
kwa vyombo vya ulinzi na usalama pale ambapo mtu anapatikana amempa ujauzito
mwanafunzi na kukatiza ndoto zao.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na kituo hiki
mapema hii leo ambapo amesema kumekuwa na changamoto katika mkoa wa njombe ya
wanafunzi kupata ujauzito wakati bado wanasoma na kukatiza ndoto zao za
kujiendeleza kielimu.
Mwamwala ameongeza kuwa mikakati ya viongozi
katika mkoa wa njombe ni kutaka mimba isiwepo mashuleni ili wanafunzi watimize
ndoto zao pia amesema kwa wanaume wanao wapa mimba wanafunzi dawa yao inachemka
na wataanza kushughulikiwa kisheria.
0 comments:
Post a Comment