Home » » Godbless Amchana Lowassa Baada ya Kwenda Ikulu na Kuonana na Rais Magufuli

Godbless Amchana Lowassa Baada ya Kwenda Ikulu na Kuonana na Rais Magufuli

Unknown | Tuesday, January 09, 2018 | 0 comments
Baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu,Edward Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu kuonana Rais Magufuli. Hatimae Mbunge wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless lema ameibuka na kusema kuwa kiongozi huyo amewakosea Watanzania kwa kauli aliyoitoa baada ya kutoka Ikulu.

Mh. Lowassa alipotoka Ikulu baada ya mazungumzo alisema kuwa; “Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo, Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga ajira, na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira, Stiegler;s Gorge ni kujenga ajira na mingine ya aina hiyo, lazima kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira, jingine ni la elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya kutosha, kwa kweli nakushukuru Mhe. Rais, you made my day,” amesema Lowassa.

Hata hivyo Lema amemhoji Mh. Lowassa kuwa ni mema gani ameyaona katika serikali hii, huku akitolea mfano Mbunge wa Singida Mashariki kuwa anauguza majeraha ya risasi.

“Mh Lowassa,umeikosea Tanzania kwa kauli baada ya kutoka Ikulu,mema yapi umeyaona katika Serikali hii?Wkt Mbunge Lissu bado anauguza majeraha ya risasi,maiti zinaokotwa,Uchumi unaanguka,Benki zinafungwa ,demokrasia imekufa Bungeni /Nje ya Bunge na Sioi mkwe wako bado yuko Magereza,” ameandika Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Advertisement
==
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG