Home » » Serikali Yaanza Kuwashughulikia Wasanii Wanaovaa Nusu Uchi

Serikali Yaanza Kuwashughulikia Wasanii Wanaovaa Nusu Uchi

Unknown | Wednesday, December 27, 2017 | 0 comments
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema wizara imeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli juu ya baadhi ya wasanii ambao wanadaiwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya kitanzania.

Waziri Mwakyembe ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari na kusema kwamba kitendo cha Rasi Magufuli kusema suala hilo, kimewapa nguvu ya kuzidi kupambana na wasanii, ambapo hapo awali walikuwa wakiwagusa huwajia juu na kulalamika.

"Pale tunapoona kuna ukiukwaji, tufumbe macho tusijali malalamiko yanavyokuja kutolewa, maana ukiwagusa wasanii walikuwa wanakuja juu sana, lakini tunashukuru mkuu wa nchi kulisemea hilo, basi na sisi tumeongezewa nguvu basi hatutaachia suala hilo kuendelea kuharibu vizazi vyetu", amesema Waziri Mwakyembe.

Hivi karibuni Rais Magufuli alizitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua wasanii wanaovaa nusu utupu kwenye kazi zao za sanaa ambazo zingine huonyeshwa kwenye television, ambazo amedai hazina maadili na zinadhalilisha utamaduni wetu na kuharibu kizazi kijacho.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG