Lissu ameyasema hayo leo mchana wakati akifanya mahojiano na idhaa ya Kiswahili ya Kijerumani (DW).
"Madaktari wangu wamenihakikishia kuwa nitarejea nchini na nitaendelea na shughuli zangu kama kawaida", amesema
Katika
hatua nyingine Lissu amesema anachokumbuka katika tukio hilo wakati
wanaingia getini kulikuwa na gari moja nyeupe limesimama huku kulikuwa
na watu wawili.
"Walikuwa
watu wawili, mmoja mwembamba niliona akishuka huku ameshika "Machine
gun" baadaye najishtukia nipo hospitali Nairobi", ameongeza.
"Ninachoshangaa ndani ya ile nyumba kuna ulinzi mkali walikuwa wapi walinzi wakati nashambuliwa", amesema.

0 comments:
Post a Comment