Nyalandu
ametumia ukurasa wake wa Facebook kutuma salamu zake za pole kwa Rais
Magufuli na familia mbalimbali za askari hao waliouwawa na wale
waliojeruhiwa katika mapigano makali yaliyotokea nchini DRC Congo
Disemba 7 na 8 kati ya askari wa Tanzania na Waasi wa Allied Democratic
Forces (ADF) yaliyopelekea askari hao 14 wa Tanzania kupoteza maisha
huku wengine 44 wakiwa wamejeruhiwa na wawili wengine mpaka sasa
hawajulikani walipo.
"Natoa pole kwa Mhe. Rais Magufuli na wanafamilia wote kufuatia kuuawa kwa maaskari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)" alindika Nyalandu

Miili
ya wanajeshi 14 wa JWTZ ambao wameuawa nchini DRC Congo imewasili leo
jijini Dar es Salaam kwa ndege maalum ya Umoja wa Mataifa, baada ya hapo
miili hiyo itapelekwa kwenye hospitali ya Lugalo kwa ajili ya kufanyiwa
uchunguzi.

0 comments:
Post a Comment