Zaidi ya watu 5,500 walikimbia
makwao nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kila siku wakati wa nusu ya
kwanza ya mwaka 2017, na kusababisha shirika moja la misaada kutaja
hali huyo kuwa mbaya zaidi.
Viwango hivyo vinamaanisha kuwa kwa
mwaka wa pili mfululizo, DR Congo ni nchi iliyoathirika vibaya na
kuhamia kwa watu kuliosababishwa na mzozo duniani, kwa mujbu wa shirika
la Internal Displacement Monitoring Centre (IDMC).
Mapigano kati
ya makundi yenye silaha, kuongezea na mzozo wa kisiasa wakati Rais
kabila amekataa kuondoka madarakani imefanya hali kuwa mbaya, mkurugenzi
wa Norwegian Refugee Council's (NRC) nchini DRC, Ulrika Blom alisema.
"Ni hali mbaya. Idadi ya watu wanaokimbia ghasia ni kubwa kuliko ya nchini Syria, Yemen na Iraq.
Licha
ya kuwepo watu milioni 4 wasio na makao na zaid ya watu milioni 7
wanaokumbwa na uhaba wa chakula msaada haijakuwa wa kutosha.
Umoja wa Mataifa ulitangaza ombi lake la juu zaidi mwezi Oktoba, lakini ni chini ya nusu ya pesa zinazohitajika zimepokelewa.

0 comments:
Post a Comment