Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Udaktari cha Imtu, Daniel Mabisi miaka 28 anadaiwa
kujinyonga hadi kufa baada ya kufeli mitihani mara mbili mfululizo.
Taarifa
zilizopatikana zinadai siku mbili kabla ya kujinyonga, mwanachuo huyo
alionekana mtaani kwao Mgeninani, Kata ya Kijichi jijini Dar es salaam
ambako jana alijinyonga majira ya saa saba mchana baada ya kutoka chuo
alikokuwa akisoma.
Akizungumza kwa simu kutoka Morogoro, baba mdogo wa marehemu, Joseph Lukuba alisema kuwa “Nimepigiwa
simu mchana huu nikaambiwa Daniel amejinyonga, nimeshtuka kwa sababu ni
juzi tu tulimtumia nauli ili arudi nyumbani Mwanza baada ya kupata
taarifa kuwa amefeli kwa mara nyingine,” alisema Lukuba.
Alisema
uamuzi aliouchukua unasikitisha kwa kuwa kufeli, isingekuwa sababu ya
kushindwa maisha hadi kufikia uamuzi wa kujinyonga.
“Kama
familia tumehama na tuko mbali kikazi, tumemuomba jirani asimamie suala
hili wakati taratibu za mazishi au kusafirisha mwili zikiendelea,” alisema Lukuba.
Akizungumzia
tukio hilo, mwenyekiti wa Mtaa wa Mgeninani, Khuruka Mwinyimvua alisema
baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kukuta mwili
ukiwa umening’inia juu ya mwembe.
“Kijana
huyo alionekana tangu juzi akizunguka mtaani hapa baada kurejea kutoka
chuoni anakosoma, alionekana kama mtu asiyekuwa na furaha,” alisema Mwinyimvua na kuongeza: “Hadi sasa mwili umechukuliwa na polisi kwa taratibu nyingine.”
Naye
kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula alithibitisha kupokea
taarifa za kujinyonga kwa kijana huyo na kuwaagiza askari walio karibu
na maeneo hayo kuchukua mwili huo.
0 comments:
Post a Comment