Upendo
Peneza amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam na kusema yeye hafurahishwi na hama hama hizo
zinazofanywa na Wabunge hao kwani zinaingiza nchi katika gharama kubwa
ya uchaguzi wa marudio ambapo fedha hizo zingeweza kutumika kufanya
maendeleo na kutatua changamoto zinazowakumba wananchi.
"Wabunge
wa majimbo kuhama kwenda chama kingine kwani unabadilika sura? Nawaomba
Watanzania wenzangu na wananchi kiujumla kama hawa viongozi na hii hama
hama inayoendelea watarudi kwa mgongo wa vyama vingine nawaombeni sana
msiwachague kwa sababu gharama zinazotumika kwenye huo uchaguzi ni
gharama ambayo ingekuletea hospitali, gharama ambayo ingeweza kununua
taulo za kike watoto wakasoma shuleni vizuri" alisema Upendo Peneza
Aidha
Mbunge huyo amewashauri wabunge wengine wa majimbo ambao wanataka
kuhama vyao vyao kuwa ni bora wasubiri na kuvumilia mpaka mwaka 2019
ambapo Katiba inawaruhusu ili uchaguzi wa marudio usifanyike na kuokoa
fedha za Watanzania.
"Pale
ambapo Watanzania wameingia gharama kwa sababu yako, pale ambapo kodi
zetu zimetumika kukuweka pale tusaidie tu mpaka baada ya miaka mitano
ikishakwisha agana nao salama au vumilia mpaka 2019 ambapo Katiba
itakuruhusu ukihama chama 2019 hatutakwenda kwenye uchaguzi mwingine
tutavumilia mpaka 2020 kwa sababu kuna muda wa kurudia uchaguzi. Kwa
hiyo nawashauri wale ambao wanataka kuunga mkono kwa kuhama wasubiri ule
muda unaoruhusiwa Kikatiba na wahame kipindi hicho ampapo nchi
haitaweza kuingia gharama yoyote ile kupata muwakilishi mpya" alisisitiza Upendo Peneza
Mpaka
sasa Wabunge wa majimbo matatu wametangaza kuhama vyama vyao na
kupoteza sifa ya kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambapo majimbo yao yatakwenda kufanya uchaguzi wa marudio siku
za usoni, wabunge hao ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Siha (CHADEMA)
Dr.Godwin Mollel ambaye amehamia (CCM), aliyekuwa Mbunge wa Singida
Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu ambaye amehamia (CHADEMA) na aliyekuwa
Mbunge wa Kinondoni Dar es salaam, Maulid Mtulia kupitia Chama cha C.U.F
ambaye amehamia (CCM).
0 comments:
Post a Comment