Mbunge
wa Iringa Mjini Chadema, Peter Msigwa amewajibu baadhi ya viongozi wa
CCM ambao wamekuwa wakisema upinzani Tanzania unakufa na kuwahoji kuwa
endapo upinzani ukifa ndiyo maendeleo ya nchi yatapatikana.
Msigwa
amesema hayo jana kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya juzi baadhi
ya viongozi wa CCM waliokuwepo kwenye Mkutano Mkuu UVCCM wa 9 ambao
ulifanyika mjini Dodoma Disemba 10, 2017 ambapo wapo baadhi ya wanachama
na viongozi wa chama hicho walikuwa wakisema kuwa kwa sasa upinzani
nchini unakufa.
“Mkutano
wa UVCCM ulibebwa na kibwagizo cha upinzani kuwa unakufa ! Fine,
tukubaliane kuwa upinzani unakufa! Ukifa upinzani zitaongezeka ajira
ngapi! Umaskini utapungua kwa kiwango gani? Haki za binadamu zitalindwa
kwa kiwango gani? Utawala bora utaimarika kwa kiwango gani ? Demokrasia
itaimarishwa kwa kiwango gani? Uhuru wa kutoa mawazo na vyombo vya
habari utaimarika kwa kiwango gani! Haya yote hayana chama! Nilitegemea
CCM mje na majibu ya haya sio upinzani unakufa” alisisitiza Msigwa.

0 comments:
Post a Comment